Posts

Showing posts from September, 2018

Bunge la SADC lasikitishwa na ajali ya kivuko, wataka sheria zifuatwe

Image
Wabunge wa  bunge  la SADC  wametuma  salamu za rambirambi  kwa Rais Dk John  Magufuli  kutokana  na vifo  vya watu zaidi ya 200  katika  ajali  ya  kivuko mkoani  Mwanza  na  wameshauri  nguvu  kubwa  kuelekezwa kwenye   usimamizi  wa  sheria za  usafirishaji  hasa wa kwenye maji  na  nchi  kavu Wakizungumza  baada ya  kutembelea Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wabunge hao  pamoja  na  kupongeza jitihada  za Rais Magufuli  kusimamia  uwajibikaji  wamesema  jitihada zaidi zinahitajika  hasa kwenye  suala zima  la  kusimamia  usalama  wa  watu  katika  sekta  za  usafirishaji. Salamu  nyingine  za  rambirambi  zimetolewa  na  baraza la biasahara la Afrika Mashariki (EABC ) kupitia  kwa mkurugenzi wake Lilian Awinja ambaye amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi  zenye sheria nzuri katika ukanda wa Afrika Mashariki kazi iliyopo ni kuzisimamia. Ziara ya  wabunge hao wa bunge la SADC katika makao makuu ya jumuiya ya Afrika  Mashariki ni  ya mafunzo na pia  kujenga  mahusiano na mashir