Posts

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande

Image
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ...

Watumishi Benki wapigwe stop simu za mikononi

Image
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa amesema matumizi ya simu binafsi za mkononi yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa mabenki wakati wa kazi, yanapaswa kudhibitiwa. Badala yake amesema, simu za mezani za ofisi zitumike wakati wote wa kazi wanapowahudumia wateja. Kutokana na baadhi ya wafanyakazi wa benki kuhusishwa na uhalifu wa kushambuliwa kwa risasi na kisha kuporwa fedha na majambazi kwa baadhi ya wateja wao, mkurugenzi huyo wa TIOB amesema matumizi ya simu binafsi kwa wafanyakazi wa benki yanatakiwa kufanyika nje ya eneo la benki baada ya kazi. “Zitumike simu za ofisi wakati wa kazi tena kwa matumizi ya kiofisi ikiwemo kuwahudumia wateja wao. Mteja anaweza kuruhusiwa kutumia simu yake ndani ya benki pale tu anapotakiwa kufanya muamala na benki husika,” alieleza Mususa alipozungumza na gazeti hili. Mususa alisema taasisi yake inahusika na kutoa masomo ya kitaaluma ya mwaka mmoja kwa wafanyakazi wa mabenki ili kuwajenga kitaaluma ...

UTATA GESTI: Wasiojulikana waua wawili chumba kimoja

Image
UTATA umeibuka baada ya miili ya watu wawili waliouawa na watu wasiojulikana kukutwa katika nyumba ya kulala wageni mjini Tanga ikiwa haina nguo na imefungwa kamba za miguu na mikononi. Katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedicto Wakulyamba miili ya watu wawili, wote wanaume, iligunduliwa jana majira ya saa mbili asubuhi na mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Kata ya Majengo jijini hapa. Kamanda Wakulyamba aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa mhudumu wa nyumba hiyo ambaye hakumtaja kwa jina, alibaini kuwapo kwa miili hiyo alipotaka kufanya usafi ndani ya chumba hicho. "Majira ya saa mbili asubuhi wakati mhudumu alipoingia ndani ya chumba hicho namba 303 kwa ajili ya kufanya usafi, alikutana na miili ya watu hao wawili wote ni wanaume ikiwa imelala chini, imefungwa kamba miguuni na mikononi," alisema. Kamanda huyo alisema miili hiyo ni ya watu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 na 40 a...

Trump uso kwa uso na viongozi wa Demokrat

Image
Trump na wanachama wa Democrats nancy Pelosi na Chuck Schumer Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na wanasiasa wawili waandamizi kutoka chama cha Demokrat katika bunge la Congress kujadili maswala tata, huku pande zote mbili zikisema mazungumzo hayo wakati wa chakula cha jioni ikulu ya white house yalikuwa yenye manufaa. Katika taarifa, Chuck Schumer na Nancy Pelosi wamesema wamekubaliana kuunda mpango wa pamoja kuhusu usalama wa mipakani na Donald Trump. Wanasema mpango huo unajumuisha kuwalinda wahamiaji wenye umri mdogo lakini haukujumuisha ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na taifa la Mexico

Mkuu wa majeshi atoa neno zito

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, amezungumzia matukio ya uhalifu wa kupiga watu na risasi yanayoendelea nchini, akisema vyombo vya ulinzi vipo kazini na hivi karibuni hali itakuwa shwari. Matukio makubwa ya watu kupigwa risasi yaliyotokea nchini hivi karibuni, ni pamoja na lile la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyepigwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na watu wasiojulikana. Jingine ni lile la Jenerali mstaafu, Vincent Mritaba, aliyepigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam akitoka benki siku tatu zilizopita. Lissu kwa sasa yupo Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu, huku hali yake ikielezwa kubadilika badilika wakati Jenerali Mritaba, anatibiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam na afya yake inaelezwa kuimarika. HALI ITAKUWA SHWARI Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Jenerali Mabeyo alisema kuwa vyombo vya ulinzi n...

Wanawake hupoteza hamu ya ngono ikilinganishwa na wanaume

Image
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia za ngono uliofanywa nchini Uingereza. Utafiti huo umebaini kwamba huku wanawake na wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu. Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya kufanya tendo la ngono. Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open. Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa. Machungu Mtaalam wa maswala ya ngono Ammanda Major amesema kuwa kwa binadamu kukosa hamu ya tendo la ngono sio swala lilisilokuwa la kawaida na kuna sababu nyingi tofauti ambazo wanaume na wanawake wanahitaji mabadiliko. ''Kwa wengine ni kawaida lakini wengine husababisha m...

Matibabu ya Lissu pasua kichwa, Sh milioni 10, Chadema yaomba msaada Ujerumani, EU

Dar es Salaam. Chadema imetangaza kuanzisha kampeni maalumu kuchangisha fedha kwa ajili ya kumgharimia mbunge wake, Tundu Lissu anayeendelea kupata matibabu mjini Nairobi huku matibabu yake yakigharimu Sh 10 milioni kwa siku. Kutokana na ukubwa wa gharama hizo chama hicho tayari kimeziomba jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU) kuangalia kama inaweza kusaidia matibabu ya mwanasiasa huyo. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdalah Safari amesema leo Ijumaa kuwa pamoja na gharama za kumtibu Lissu kuwa kubwa lakini chama kitaendelea kumpigania ili kuokoa maisha yake. “Unajua chama tumepoteza watu wengi sana, kama vile Ben Saanani, Dk Slaa ( Willbroad) lakini tuna mahaba makubwa na ndugu yetu Lissu hivyo tunaendelea kupigania maisha yake. Gharama  anazotumiwa kutibiwa ni kubwa mno maana kwa siku inagharimu kiasi cha Sh10 milioni sasa sisi peke yetu hatuwezi ndiyo maana tumeamua kuomba msaada toka kwa rafiki zetu,” amesema. Amesema chama kimeunda k...