Chimbuko la Illuminati na dhana kuhusu nguvu zao
Haki miliki ya picha ALAMY Image caption Baadhi huamini michoro iliyo kwenye dola za Marekani ina uhusiano na Illuminati Ni simulizi ya ulaji njama ambayo bila shaka imevuma zaidi kushinda njama nyingine zote. Ni wachache sana ambao hawajawahi kusikia kuwahusu Illuminati. Huaminika kuwa kundi maalum la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia, na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia. Kwa wengine, wamehusishwa na utajiri wa ghafla ambao si wa kawaida. Ukitajirika haraka, kunao bila shaka watakaodai kwamba umejiunga na Illuminati. Je, kuna ukweli wowote kuhusu wasiwasi huu? Kuna kundi la watu wanaofanya vikao vya siri kupanga njama za kuitawala dunia na pia kjifaidi wenyewe kwa pesa na utajiri? Simulizi hizi na umaarufu wa illuminati zina ukweli wowote? Wasiwasi huu kuhusu kundi linalopanga njama ya kuweka utawala mpya duniani ulianza miaka ya 1960, sana kutokana na ubunifu wa watu fulani. Kuenea kwa habar...