Posts

Showing posts from August, 2017

Pastor Chris The Value of time 226 X 400

Image
 THAMANI YA MDA ULIO NAO SASA NA matumizi yake tizama hapa uone umuhimu wa muda sas na hata baadae kwani muda hautosubiri binadamu kwa ukitoka ndo usha  enda haurudi tena

WHO ARE YOU

Image
                                                                                                                                                             Always we as human being, we are suffering from difference circumstances but when we already know what does those challenges means we can’t give up. From the beginning we were created to suffer so don’t give up. Self-confidence, self-worth, self-control, as well as determination are needed to everyone, they will help you to know, who are you, where are you coming from, where are you, where are you going, what do you want, who you want to be and all in all they will help you to build your future. Don’t say tomorrow I shall do just start now, Because every second,minute,hour,day,week,mounth as well as year when passed does not coming back. To building the future want sacrifice on what you want. HAVE THE NICE DAY MY DEAR

Serikali yamwaga ajira mpya Kibiti

Image
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani imetangaza nafasi 45 za ajira kwa wanaotaka kuwa watendaji wa vijiji wilayani humo. Imesema imetangaza ajira hizo, ili kupata watendaji wa vijiji watakaoziba mapengo ya waliofariki na walioachishwa kazi kutokana na kuwa na elimu ya darasa la saba. Kibiti ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Pwani ambazo kwa miaka miwili iliyopita, zimekumbwa na mauaji ya viongozi wa ngazi mbalimbali, wakiwamo watendaji na wenyeviti wa vijiji. Mauaji hayo yalikuwa yakitekelezwa na watu wasiofahamika, waliokuwa wakivamia nyumba za watendaji hao na kuwaua kwa kuwapiga risasi. Wilaya nyingine za mkoa huo zilizokumbwa na mauaji hayo ni Rufiji na Mkuranga. Aidha, kutokana na kushamiri kwa mauaji hayo na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na wauaji, baadhi ya watendaji wa vijiji waliripotiwa kukimbia makazi yao wakihofu kuuawa. Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye, alisema hali

Zijue faida za uaminifu katika mahusiano ya Ndoa

Image
Suala la uaminifu katika mapenzi kwa karne hii limekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi sana, wengi wemekuwa si waaminifu wakati mwingine kupelekea mahusiano hayo kufa. Hivyo uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi kwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuna faida nyingi kwa mwili na akili. Watu walio katika mahusiano bora ya mapenzi huishi maisha marefu na kufurahia afya njema kuliko wale wasiokuwa katika mahusiano ya aina hiyo. Faida hii haina pingamizi kwa sababu ya ukweli kwamba watu wanaokuwa katika mahusiano ya karibu wanajijengea hisia na nguvu fulani ambayo huwasaidia kusaidiana na kujaliana wakati wa shida. Siyo tu kwamba watu walioko katika mahusiano ya aina hii wanaishi muda mrefu lakini pia ni kweli kwamba wanakuwa na furaha na wanaridhika na maisha kuliko wale wanaoshindwa kukaa katika mahusiano. Pili, kuwa katika mahusiano mazuri ya mapenzi kunasaidia katika mambo mbalimbali ya kimahitaji. Kusaidiana katika mahitaji mbalimbali baina ya wapenzi ni njia nz

Makosa wanayofanya wanawake katika mahusiano ya kimapenzi

Image
Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia mahusiano mengi ya kimapenzi kufa, na miongoni mwa tabia hizo ni pamoja na zile tabia ambazo wanawake hao wamekuwa wakiziendekeza na miongoni mwa tabia hizo ni kama ifutavyo; Kauli mbaya kwa mmewe .  Unakuta mwanamke anaropoka mbele ya mme wake utafikiri kafingiwa mota mdomoni. Uchafu.   Unakuta baadhi ya wanawake akioga usiku mpaka usiku mwingine. Nguo ya ngani ukiangalia utafikiri mafundi wamepiga plasta ukuta. Kukataa kufanya tendo la ndoa wakisingizia wamechoka. Dharau. Kuto mueshimu mwanaume na kuona hana kitu kwake wala hamsikilizi kwa lolote na maamuzi yandani hupanga yeyey akjisema mumwe wala hata hajari Kuwa na michepuko ya wanaume wa nje . Pesa.   Wanawake wakipata pesa uona wanaume wao si lolote. Elimu .  Mwanamke akisoma na kumzidi mmewe basi anaona hata tendo la ndoa kufanyika maamuzi ni yake mwenyewe. Upatikanaji wa elimu kwa mwanamke umesababisha mahusiano mengi kufa. Madaraka .  Ukifanya ut

ujiepushe Kunywa Maji Baridi Yana Madhara Kwa Afya Ya Binadamu

Image
MADHARA YA KUNYWA MAJI BARIDI UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku. Pamoja na ukweli kwamba maji baridi ni;matamu', lakini siyo mazuri kwa afya yako na katika makala ya leo tutaangalia ukweli kwa nini maji haya siyo mazuri. Kwa mujibu wa utafiti uliokwisha fanywa na wataalamu  wa masuala ya lishe, mtu anapokunywa maji baridi mara baada ya kula chakula, maji yale yanapopita kwenye utumbo huchangia kugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula. Kitendo hicho, husababisha usagaji wa chakula kuwa wa taratibu sana na hivyo kuchangia ukosefu wa choo. Mbali na ukosefu wa choo, ambao ni madhara yanayojionesha kwa muda mfupi, lakini pia kuna madhara ya muda mrefu yanayoweza kujitokeza baadaye sana. Inaelezwa zaidi kuwa, wakati chakula kinapochelewa kusagwa kwa sababu ya kuga

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Image
Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni      Introvant: watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina                  hapa kuna makundi mawili 1. Melancolin              2. Fragmetic 2.      extrovants: wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao Hapa kuna makundi mawili 1.  Sanguine           2. Colerick Na sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao 1.MELANCOLIN Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo -wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient) -ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi -wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu -ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi -wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati -Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana ha

Njia za Kujikinga na Magonjwa ya Moyo

Image
Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases) yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika nchi za Afrika kinyume miaka ya nyuma. Kati ya sababu mojawapo ni mabadiliko katika mitindo ya maisha na lishe. Watu wengi hawana mazoezi na wanakula vyakula vyenye nishati nyingi (energy dense diet) kuliko vyenye virutubisho kwa wingi (nutrient dense diet), na hili linachangia sana kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa haya. Labda unajiuliza ni magonjwa gani haya? Hapa tunaongelea magonjwa kama shinikizo la damu la kupanda (presha au hypertension), kiharusi (stroke), moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure), moyo kuwa mkubwa, shambulio la moyo (heart attack) na mengineyo. Zikiwemo sababu nyingine, magonjwa haya kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mitindo ya maisha na lishe. Njia Za Kuzuia Magonjwa Ya Moyo Na Mishipa Ya damu Kwa kubadili mtindo wako wa maisha unaweza kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, au usiyapate kabisa. Zingatia mambo yafuatayo kujikinga na magonjwa