Posts

Showing posts from October, 2017

SAIKOLOJIA : Je, unazijua mbinu za kushawishi?

Kwa ufupi Au unaweza kushawishi katika mambo makubwa kama vile kuwashawishi wafanyakazi au wafanyabiashara wenzako muwe mkichanga fedha kila mwezi na kumpatia mmoja wenu kwa zamu ili kusaidiana kupunguza makali ya maisha. Je katika maisha yako ya kila siku huwa unafanikiwa kumshawishi mtu kufanya jambo fulani? Linaweza kuwa jambo dogo tu kama vile kumshawishi mtu akuazime kalamu yake uandikie kwa sababu ni nzuri. Au unaweza kushawishi katika mambo makubwa kama vile kuwashawishi wafanyakazi au wafanyabiashara wenzako muwe mkichanga fedha kila mwezi na kumpatia mmoja wenu kwa zamu ili kusaidiana kupunguza makali ya maisha. Labda nikuulize swali kwa upande mwingine. Je mara ngapi watu wengine huwa wanakushawishi wewe kufanya jambo fulani? Je wauzaji wanaotembea barabarani au nyumba hadi nyumba wamewahi kukushawishi kununua bidhaa zao? Je marafiki au ndugu zako wamewahi kukushauri kuacha tabia fulani kama vile kunywa pombe au kukushawishi utende jambo jipya kwako kama vile kuji

Wekeza Kwa Shilingi Laki Moja, Upate Zaidi Ya Milioni Moja Na Nusu Ndani Ya Siku 90

Image
Leo nataka tuangalie kilimo cha matikiti kibiashara kwa mtaji wa shilingi laki moja tu(100,000/=). Nimeona niandae hili somo kwa kuwa watu wengi hulalamika kuhusu mtaji lakini kwa asilimia kubwa watu humililiki zaidi ya hii pesa laki moja, lakini bado utamkuta analalamika kuhusu mtaji wa kuanzia. Leo tutaangalia mchanganuo wa shilingi laki moja ili ikuletee milioni moja na nusu(1,500,000/=) kwa makadilio ya chini kabisa hayo ni baada ya siku 75-90 na unaweza pata zaidi ya hapo, ikiwa utaweka juhudi nyingi katika kilimo ambacho unaenda kufanya. Hapa tutaangalia mchanganuo kwa kutumia mbegu bora ya matikiti aina ya PATO F1. Na eneo linalohitajika ni chini ya robo ekari (yaani nusu ya robo ekari ) ila katika laki moja sijaweka gharama ya shamba ambayo ni nusu ya robo ekari yaani mita 500 za mraba. Maandalizi ya shamba. Andaa shamba lenye ukubwa wa mita 500 za mraba( 50m×10m). Baada ya kuliandaa shamba lako hakikisha una mbolea ya kuku ya kutosha mashimo 500 tu na uhakikishe hiyo mbolea

Chanzo cha saratani ya matiti

Image
Hakuna kitu kingine kizuri kama mwili wa mwanamke kwakuwa unaweza kuleta kiumbe binadamu kingine. Mwili wa mwanamke unazo ovari ambazo hutengeneza mayai na homoni maalumu ambazo hudhibiti mwili wake wakati wa ujauzito kuanzia wakati yai linaporutubishwa mpaka mwishoni mwa wastani wa miezi tisa (wakati wa kujifunguwa). Mfumo huu maalumu huanza kazi mara mwanamke anapoanza mzunguko wake wa uzazi (mzunguko wa hedhi). Kwa wastani kila siku 30 ovari zake zitazarisha yai na kuliweka katika mfumo wake wa uzazi likisubiri kurutubishwa. Wakati yai hili limetolewa, mwili wake utaanza kujiandaa kwa uwezekano wa kupata mtoto. Mfuko wa uzazi (uterus) utaanza kubadili uundwaji wake wa seli kwa kuandaa uwezekano wa kukishikilia kijusi (fetus) baada ya yai kurutubishwa. Wakati yai litakapokuwa limerutubishwa ovari zake (mwanamke) zitachukuwa majukumu ya mwili wake na kuhakikisha kuwa kijusi kinapata kile kinachokihitaji ili kuishi. Ubongo wa mwanamke pia huathiriwa kutokana na kutolewa kwa homoni

Lishe Bora kwa Maisha Yote

Image
Inajulikana kabisa kuwa nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko wa vitu vingi. Nyumba hii huonekana nzuri na yenye kupendeza wakati wote na pia haimomonyoki kirahisi wakati wa mvua au upepo mkali. Nyumba imara hujengwa kwa mchanganyiko kama wa cementi, mchanga, kokoto, nondo n.k. mchanganyiko huu huwa katika kiwango sahihi, hii ni kwamba kuna kiasi au uwiano sahihi katika mchanganyiko huu. Kimojawapo kati ya hivi kikipelea au kuwa katika kiasi pungufu basi nyumba haitakuwa imara, vilevile kimojawapo kikizidi basi nyumba haitakuwa imara pia. Hivyo nyumba ili iwe imara ni lazima mchanganyiko huu uwe katika uwiano ulio sahihi. Mpaka hapo swali linakujia, je mwili wako unajengwa na nini? je kuna uhitaji wa uwiano sahihi? Mwili wa binadamu hujengwa kwa chakula. Chakula hicho ni lazima kiwe chakula bora au mlo kamili. Mlo kamili unajumuisha makundi matano ya vyakula ambayo ni: nafaka, mizizi na ndizi, kundi la pili: vyakula vyenye jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyama, kundi la tatu:

Hizi ndizo Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya

Image
Ni matumaini nyote mnaendelea vyema,  Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu na ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni, leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK, ~Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo ~Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria ~Kwa

Fahamu Aina 61 Za Ubanaji Wa Nywele

Image