SAIKOLOJIA : Je, unazijua mbinu za kushawishi?



Kwa ufupi
Au unaweza kushawishi katika mambo makubwa kama vile kuwashawishi wafanyakazi au wafanyabiashara wenzako muwe mkichanga fedha kila mwezi na kumpatia mmoja wenu kwa zamu ili kusaidiana kupunguza makali ya maisha.
Je katika maisha yako ya kila siku huwa unafanikiwa kumshawishi mtu kufanya jambo fulani? Linaweza kuwa jambo dogo tu kama vile kumshawishi mtu akuazime kalamu yake uandikie kwa sababu ni nzuri. Au unaweza kushawishi katika mambo makubwa kama vile kuwashawishi wafanyakazi au wafanyabiashara wenzako muwe mkichanga fedha kila mwezi na kumpatia mmoja wenu kwa zamu ili kusaidiana kupunguza makali ya maisha.
Labda nikuulize swali kwa upande mwingine. Je mara ngapi watu wengine huwa wanakushawishi wewe kufanya jambo fulani? Je wauzaji wanaotembea barabarani au nyumba hadi nyumba wamewahi kukushawishi kununua bidhaa zao? Je marafiki au ndugu zako wamewahi kukushauri kuacha tabia fulani kama vile kunywa pombe au kukushawishi utende jambo jipya kwako kama vile kujiunga na siasa? Ushawishi wa aina hii ambao humfanya mpokea ujumbe aamini jambo fulani au atende kitendo fulani huitwa mawasiliano ya ushawishi. Wengi wetu hutumia wakati wetu mwingi katika mawasiliano ya ushawishi.
Lakini hebu tujiulize “Ushawishi maana yake nini?” Ushawishi unaweza kutafsiriwa kama ni mawasiliano yenye lengo mahsusi la kubadilisha mawazo ya mpokeaji ujumbe au kumsukuma kufanya jambo fulani. Mtoa ujumbe wenye lengo hili hutumia mkakati unaoathiri fikira na vitendo vya anayetumiwa ujumbe. Ili kufanikisha lengo hili ni lazima mtoa ujumbe alenge ujumbe wake kushawishi kwa mlengwa au walengwa wanaokusudiwa.
Jinsi ya kushawishi
Je tunakubali kwamba watu wanaweza kushawishiwa kufanya jambo fulan? Hebu wewe mwenyewe jaribu kukumbuka ni lini uliwahi kumshawishi mtu kufanya jambo fulani ukafanikiwa? Unafikiria ni kitu gani kilikufanya ufanikiwe kumfanya abadili mawazo au tabia. Tena jaribu kufikiria kwa upande wako. Kama uliwahi kushawishiwa na ukashawishika kubadili fikra au kufanya vitendo fulani aliyekushawishi alitumia njia au mbinu gani kukufanya ubadili mawazo yako ya kufanya mambo kinyume na jinsi ulivyozoea.
Unapotaka kumshawishi mtu inabidi uiweke akili yake katika mgongano wa mawazo au fikra zisizopatana. Kuna mfano ambao wanasaikolojia wengi hupenda kuutumia.
Inafahamika kuwa kila mtu hupenda kufikiriwa kuwa yeye ni muungwana. Lakini siyo kweli kuwa kila anayedhani yeye ni muungwana ni muungwana kweli. Mshawishi anaweza kumuonyesha mtu kuwa yeye siyo muungwana kwa kusababisha mgongano wa mawazo katika akili yake. Kwa mfano anaweza kukuuliza “Je unafiria mtu anaweza kuwa muungwana kweli kama hapendi kujumuika na watu wa hali ya chini ili kujenga ujamaa?” Swali hili linaweza kuwa changamoto kwa kila anayedhani kuwa yeye ni muungwana. Anaweza kubaini kuwa yeye siyo muungwana thabiti kwa kuwa amepewa mawazo kuwa muungwana wa kweli ni yule ambaye huwa anapenda kujichanganya na watu wa hali ya chini bila kuwabagua. Kwa upande mwingine, swali hili pia linaweza kuwa kichocheo cha ushawishi wakati mpokeaji wa ujumbe atakapowaza kuwa “sina budi kuchanganyika na watu wa hali ya chini ili niwe muungwawa kweli. Licha ya kuwa muungwana nitaweza pia kuimarisha ujamaa”
Huu ni mfano wa mgongano wa mawazo unaotoka nje, lakini kunaweza kuwa na mgongano wa mawazo katika akili ya mtu mwenyewe.
Hebu tuchunguze mfano huu mtu anaweza kuwa na mgongano wa mawazo katika akili yake mwenyewe. Mgongano wa mawazo baina ya kile anachokusudia kufanya na kile ambacho angestahili kukifanya. Kijana mmoja aliye masomoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikuta amechanganyikiwa mawazo kama hivi.
Siku fulani timu maarufu ya mpira wa miguu kutoka nje iliwasili nchini kupambana na timu ya Taifa ya Tanzania. Kwa kuwa kijana huyo ni shabiki wa mpira alitamani kwenda kuiona mechi hiyo ya kihishoria. Lakini siku hiyo ya mechi hiyo yaani Jumapili alikuwa amepanga kujisomea kwa ajili ya mtihani uliokuwa umepangwa ufanyike siku ya pili. Sasa alikuwa anashindwa kuamua aache kujisomea au aende mpirani na kubakia na muda mfupi wa kujisomea usiku.
Mara akatokea rafiki yake ambaye pia angependa kwenda naye mpirani. Hivyo, anaanza kwa kumshawishi kuwa hata kama akienda mpirani atakaporudi bado atakuwa na muda wa kutosha kwa kujisomea. Hoja ya pili anayoitumia ni kumweleza kuwa mtihani wa siku ile haukuwa mkubwa na kwamba una alama kidogo tu katika matokeo ya mitihani yao yote. Hoja ya tatu anayoitumia kwa kumshawishi anasema “Hata kama ukichelewa unaweza kuamka mapema alfajiri kujisomea” Huyu rafiki yake anamshawishi kwa kufanya mambo mawili. Kwanza alijaribu kumwelekeza jinsi atakavyoweza kutatua mgongano wa mawazo. La pili alilofanya rafiki yake lilikuwa ni kumrubuni atatue mgogoro wa mawazo yake kwa kufuata ushawishi wake kwa sababu yeye alikuwa akipenda waende pamoja mpirani.
Kumbuka unapotaka kumshawishi mtu yeyote huna budi kutambua kuwa, kwa kawaida ni vigumu kwa mtu kusikiliza ushauri au ushawishi na kukubali mara moja kubadili tabia. Watu huona ni bora wabakie na imani zao kama zilivyo tu. Hivyo unapokuwa unataka kushawishi ni lazima uufanye mgongano wa mawazo uonekane ni mkubwa na wa kweli. Nakumbuka babu yangu ambaye hakusoma shule alikuwa haamini kabisa kama ni muhimu binadamu kula mboga za majani. Hebu fikiria ungeweza kujenga mgongano wa mawazo wa aina gani ambao ungemshawishi hasa kwa jinsi alivyokuwa anapendelea nyama na samaki. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu zinaweza kutumika kwa kushawishi.
1. Kuponda au kukihafifisha kitu fulani, kukipamba na kukipandisha hadhi kingine
Hii ndiyo njia rahisi inayotumika zaidi kuliko nyingine zozote za ushawishi. Unapotaka kumshawishi mtu fulani kupenda au kutenda jambo fulani ni lazima uwe na jambo jingine lilsilofaa ambalo utalitumia kwa kulilinganisha na lile bora ili kuonyesha tofauti.
Mathalani unapomshawishi mtu kuacha kunywa pombe huna budi kutumia mifano ya maisha ya watu wawili tofauti mmoja awe yule mlevi wa pombe na yule wa pili awe asiyekunywa kabisa pombe. Kwa hakika kushawishi ni kazi ya kupandisha thamani na ubora wa kitu kimoja na kushusha thamani na kukikashifu kitu kingine.
2. Kurudiarudia kunadi jambo tarajiwa
Hakuna mbinu yenye nguvu ya ushawishi kama ile ya kurudiarudia ujumbe masikioni au machoni mwa mlengwa au vyote kwa pamoja yaani masikioni na machoni kwa wakati mmoja. Mbinu hii hutumiwa sana na wafanyabiashara. Kwa mfano wanapotaka kuwashawishi watu wanunue sabuni ya aina fulani, watahakikisha ujumbe wa kuisifia sabuni hiyo unawekwa katika kila chombo cha habari kama vile magazeti, redio, televisheni na pengine hata kwenye mabango. Matangazo hayo yatatolewa mara nyingi sana ili watu wayasikie au kuyaona tena na tena hadi akili na mawazo yao yashawishike na akili zao ziamini kuwa hakuna sabuni nyingine iliyo nzuri kuliko hiyo.
3.Kuhusianisha jambo au kitu fulani na kingine
Mshawishi anayetumia mbinu hii hujitahidi kuhusianisha wazo, mtu au bidhaa anayotaka kuifanyia ushawishi na kitu kingine ambacho mpokeaji wa ujumbe anakipenda na anakihitaji.
Na kama nia ni kumfanya akichukie au akiache kitu fulani, mshawishi hana budi kukilinganisha na kile kitu ambacho mlengwa wake hakipendi kabisa na pengine hata anakiogopa.amemshawishi kuifuata. Ili kufanzaidi kuliko kingine alichokusudia kukitumia kama kielelezo cha ubora.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri