Posts

Showing posts from December, 2017

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MULUNGUSHI:

Image
                            KANISA LA WAADVENTISTAWASABATO MULUNGUSHI -IGOGO                                                                          MWANZA.                                                        Wanayo furaha kukualika/kuwaalika. Bw/bi/mhe./Dkt./mch./mwl./ndg …… Kwenye changizo la kununua viti vya kanisa. Litakalo fanyika trh,20/01/2018,siku ya jumamosi (SABATO) katika kanisa la wasabato Mulungushi, kuanzia saa 08:00-mchana hadi saa 11:30 jioni. Lengo ni kupata kiasi cha sh.10,000,000/=(Millioni kumi). Viti-500 Sh.5,000,000/= Mic- 15 Sh.2,000,000/= Kuvuta umeme Sh.700,000/= Speaker -2 Sh.2,300,000/= Jumla Sh.10,000,000/= Nimatumaini yetu kuwa utashirikiana nasi kufanikisha lengo hili katika kazi ya MUNGU kwa njia ya matoleo.                        Mungu akubariki unapo jiandaa kushirikiana nasi Emmanuel Shadrack   

Maji ya kale zaidi duniani yagunduliwa Canada

Image
Haki miliki ya picha UTORONTO Image caption Maji hayo yaligunduliwa kilomita 3 chini ya ardhi kwenye mgodi Canada Wanasayansi nchini Canada wamegundua maji yanayoaminika kuwa ya kale zaidi duniani, ambayo wanaamini yamekuwepo angalau kwa miaka bilioni mbili. Maji hayo yamegunduliwa katika mgodi uliopo nchini Canada. Wanasayansi walikuwa wamegundua maji mengine mwaka 2013 eneo hilo yaliyokadiriwa kuwa ya kutoka miaka 1.5 bilioni iliyopita lakini sasa wanasema maji waliyoyagundua karibuni ni ya zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita. Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Toronto waliwasilisha matokeo ya utafiti wao katika mkuano wa wataalamu wa fizikia ya dunia mjini San Franc Profesa Barbara Sherwood Lollar, aliyeongoza wataalamu waliofanya ugunduzi huo aliambia BBC: "Watu wanapofikiria kuhusu maji haya, wanafikiri labda ni matono ya maji yaliyokwamba ndani ya jiwe. "Lakini haya ni maji yanayotiririka. Yanatoka kwa kasi ya lita kadha kila dakika - ni maji mengi sana

Lugha inayozungumzwa na watu watatu pekee Afrika

Image
Image caption Katrina Esau anafanya kila awezalo ili lugha yake ya utotoni linasalia duniani hata baada ya kifo chake Katrina Esau anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa lugha yake asili, ambayo kwa sasa inazungumzwa na watu watatu pekee, haiangamii. Bi Esauni, 84, ni mmoja wa watu watatu walio hai ambao wanazungumza kwa ufasaha lugha iitwayo N|uu, mojawapo ya lugha zinazozungumzwa nchini Afrika Kusini ya jamii ya San, ambao pia wanafahamika kama Bushmen. Lugha ya N|uu inachukuliwa kama lugha asili ya taifa la Afrika Kusini. Huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye anaweza kuzungumza kwa ufasaha lugha hiyo isipokuwa watu wa familia yake, lugha hiyo imetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama "lugha iliyo katika hatari kubwa ya kuangamia". "Nilipokuwa mtoto, nilikuwa nikizungumza tu Ki- N|uu na nikawasikia watu wengi mno wakiongea lugha hii. Ilikuwa ni habari njema, tuliipenda sana lugha yetu, lakini hilo kwa sasa limebadilika," anasema Bi Esau huko Upington, m

Umasoni: Wanawake ambao ni wa Freemason na itikadi zao

Image
Image caption Gunge Mkuu Zuzanka Penn ana cheo cha juu zaidi miongoni mwa Freemason wanawake England Wanawake wa Freemason wamekuwa wakikongamana kwa zaidi ya miaka 100 sasa - wakifanya matambiko na sherehe sawa na wenzao wa kiume. Lakini si watu wengi wanaofahamu kuwepo kwa kundi hili. Sasa tunaweza kukufahamisha zaidi kuhusu shughuli za Freemason hawa wa kike baada ya kipindi cha redio cha Victoria Derbyshire cha BBC kuruhusiwa kuzungumza nao. "Freemason ni nani?" anauliza mmoja wa viongozi wao ambao huitwa master (gunge) katika Kongamano Tukufu la Jumuiya ya Freemason wa Kale. "Ni mfumo wa kipekee wa maadili ambao umezingirwa na istiari na ishara zenye maana," anajibu Dialazaza Nkela. Nkela anashiriki katika sherehe ya kipekee ya kumfikisha ngazi ambayo hufahamika kama "shahada ya pili". Ni sherehe ya kusherehekea kupanda hadhi kwake katika kundi lake. Kufikia kwake "shahada ya kwanza" kuliadhimishwa kwa kuingizwa kwake katika