Njia zitakazokusaidia kuwa na furaha katika maisha yako ya kila siku


Mabadiliko yaliyo mepesi  kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka, hivyo kila wakati ni lazima uweze kutafakari na kufikiri vyema ni kwa namna gani unaweza kuwa na furaha na amani ndani ya moyo wako.

Zifutazo ndizo njia za kuwa na furaha katika maisha yako;

Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku.
Kulala usingizi wa kutosha  unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala,  usitumie chakula kingi wakati wa jioni.

Jitahidi kuamka mapema
Kama wewe ni mfanyakazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema  dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako.

Fanya tafakari 
Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo  ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na  hutachanganyikiwa na kazi zako.

Jifunze kitu kipya
Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hiyo ndiyo changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha  afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa haraka kwa kile ukifanyacho.

Tembea mara kwa mara
Kutembea kwa dakika 30 kwa siku  moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira,  hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi .

Usijihusishe sana na mambo ya mitandao.
Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya.

Kuwa mwema.
Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri