Utokaji mimba na Visababishi vingine vya Kuvuja damu mapema katika Ujauzito

Kipindi cha utokaji mimba na Visababishi vingine vya Kuvuja damu mapema katika Ujauzito

Utangulizi

Katika kipindi hiki utajifunza kuhusu visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito, yaani mwanamke anapovuja damu akiwa mjamzito na kabla ya wiki 28, na halipaswi kutendeka. Kutoka kwa mimba ni mojawapo ya visababishi vya kawaida sana vya kuvuja damu mapema katika ujauzito na ni sababisho kuu la vifo vya kina mama na maradhi yanayohusiana na kuzaa ulimwenguni. Aidha, kati ya mimba 100, 15 hutoka pekee yao (uharibikaji wa mimba). Utajifunza jinsi ya kuainisha utokaji wa mimba ili kutoa utunzaji unaofaa, na mtazamo wa kisheria kuhusiana na utoaji wa mimba na njia salama za kutoa mimba zinazotumika katika vituo vya afya. Mimba isiyo kuwa ya kawaida na katika sehemu yake ni visababishi vingine vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito. Mwanamke anaweza kuwa na matatizo ya kiafya akimaliza ujauzito mapema, kwa hivyo unapaswa kujua ishara za onyo. Kipindi hiki kinamalizia na jukumu la kumshauri kuhusu utunzaji wa dharura na rufaa ya awali ambayo inaweza kuokoa maisha ya mwanamke, na ushauri baada ya kutoa mimba na upangaji uzazi.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 20

Baada ya somo hili, unapaswa kuwa na uwezo wa:
20.1 Kufafanua na kutumia kwa ufasaha maneno yote muhimu yaliyoandikwa kwa herufi nzito. (Swali la Kujitathmini 20.1)
20.2 Eleza visababishi vya kawaida vya uvujaji damu katika mimba ya mapema. (Swali la kujitathmini 20.2)
20.3 Eleza uainishaji wa dalili za utokaji mimba, mtazamo wa kisheria, na njia salama zinazotumika katika vituo vya afya kutoa mimba. (Swali la Kujitathmini 20.1 )
20.4 Tambua ishara za onyo na matibabu ya dharura yanayohitajika kabla ya rufaa ya kuvuja damu mapema katika ujauzito. (Swali la Kujitathmini 20.2)
20.5 Eleza sifa za utunzaji baada ya kutoa mimba salama kwa mwanamke, pamoja na huduma ya upangaji uzazi. (Maswali ya Kujitathmini 20.1 na 20.3)

20.1 Je, kuvuja damu mapema katika ujauzito ni nini?

Kuvuja damu kabla ya wiki 28 za ujauzito hudhaniwa kuwa ni kuvuja damu mapema katika ujauzito. Ikitokea baada ya wiki 28, huitwa utokaji wa damu wa baadaye katika ujauzito. Mkato huu wa wiki 28 umezingatia uwezekano wa kuishi ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya tarehe iliyotarajiwa katika wiki 28. Matumaini ya kuishi kabla ya wiki 28 ni madogo sana katika nchi nyingi zinazoendelea maana kuna upungufu wa vifaa vya afya vya utunzaji maalum kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Siku hizi nchi zingine zimepunguza mkato huu hadi wiki 20 kwa sababu ya utunzaji ulioimarishwa na teknolojia inayotolewa na mfumo wao wa afya.
Visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito ni utoaji wa mimba, kutoka kwa mimba mapema kwa sababu ya kufa kwa fetasi. Visababishi vingine viwili vya kawaida ni mimba iliyotungwa nje ya uterasi (Wakati fetasi hujitia na kukua nje ya uterasi), na mimba isiyokuwa ya kawaida (wakati uvimbe unakua katika uterasi badala ya fetasi). Tutarejelea matatizo haya tukikaribia mwisho wa kipindi hiki, lakini lengo letu kuu ni uavyaji mimba.

20.2 Uavyaji mimba

20.2.1 Mimba kutoka pekee yake

Mimba kutoka pekee yake (kuharibika kwa mimba) hutokea kwa kawaida katika 15% ya mimba, wakati mwingine hutokea mapema sana kiasi cha kuwa mwanamke hawezi kufahamu kuwa alikuwa mjamzito. Hata hivyo, kuharibika kwa mimba pekee yake wakati mwingine inaweza kusababisha uvujaji wa damu nyingi na kuhatarisha maisha ya mwanamke. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa, jeraha, vurugu, malaria na mafadhaiko yanaweza kufanya mimba kutoka mapema. Wakati mwingine mimba huharibika kwa sababu mwanamke amekuwa karibu na sumu au kemikali zilizo na toksini. Si rahisi kujua kila wakati kinachosababisha uharibikaji wa mimba, lakini visababishi vingine vya kuharibika kwa mimba vinaweza kukingwa. Kuharibika kwa mimba wakati mwingine unaweza kukingwa kwa kutibu wanawake kutokana na maradhi na maambukizi na kuwasaidia kuepukana na sumu ya kemikali na vurugu. Lakini wanawake wengine huwa na uharibikaji wa mimba mmoja baada ya nyingine, na huweza kushindwa kujua ni kwa nini.
 Wanawake walio na historia ya uharibikaji wa mimba unaojirudia wanapaswa kutibiwa katika kituo cha afya kilicho na huduma za kipekee ili kutafuta sababisho na kuwasaidia kubeba mimba hadi mwisho wa ujauzito.

20.2.2 Utoaji mimba wa kupanga

Mimba zisizopangwa na zisizotarajiwa, hasa katika wasichana wanaobalehe, zinaweza kusababisha mwanamke kukimbilia utoaji mimba wa kupanga(kukomesha ujauzito kimakusudi). Katika hali fulani kwa nchi zingine, utoaji mimba ulioruhusiwa unaweza kutekelezwa kwa usalama katika kituo cha afya na mhudumu wa kiafya aliyehitimu. Utaratibu huu kwa kawaida hauhatarishi ujauzito wa siku sijazo wa mwanamke. Msimamo wa kisheria na njia zinazokubalika za kutoa mimba kwa usalama zimeelezwa katika kitengo 20.2.4 cha kipindi hiki.
Mchoro 20.1 Utoaji mimba usio salama unaweza kusababisha kuvuja damu nyingi, maambukizi hatari, ukosefu kuzaa tena au hata kifo.
Utoaji mimba usiokuwa salama ni mimba unaotolewa na mwanamke mwenyewe au na mtu asiye na ujuzi katika mazingira safi chafu (Mchoro 20.1).
Mwanamke aliyekuwa mgonjwa, aliyejeruhiwa, au aliyevuja damu nyingi baada ya kutoa mimba anaweza kuwa na kovu katika uterasi zinazoweza kusababisha matatizo katika ujauzito wa siku sijazo. Kifo kutokana na utoaji mimba usiokuwa salama ni mojawapo ya visababishi vya vifo na maradhi kwa kina mama ulimwenguni vinavyoongoza hasa katika nchi zinazokuwa. Ni sababisho kuu la vifo kwa kina mama na linahitaji kushughulikiwa ili kupunguza vifo vingi kwa kina mama nchini.

20.2.3 Uainishaji wa dalili za utoaji mimba

Matokeo ya mimba kutoka pekee yake au utoaji wa mimba uliopangwa yameainishwa kwa kuzingatia mawasilisho ya kliniki, kama ilivyoamuliwa na mhuduma wa afya. Ni muhimu kujua aina tofauti, kwa sababu utakavyomtibu mwanamke hutegemea na uainishaji wa kliniki.
Utoaji mimba uliokamilika
Utoaji mimba uliokamilika inamaanisha kuwa sehemu zote za fetasi na plasenta zimetolewa kupitia uke; hakuna kilichobaki katika uterasi na seviksi imefungika. Hakuna utaratibu wa matibabu wa kutoa kila kitu (tupu) kwa kawaida huhitajika. Baada ya utoaji mimba uliokamilika ambao ulitekelezwa kwa usalama mwanamke anaweza kuhisi maumivu madogo katika fumbatio lake, na uvujaji damu kutoka ukeni unapaswa kuwa kama hedhi ya kawaida.
 Ikiwa uvujaji damu ni karibu wastani, na kunazo tishu za fetasi zinazotoka kupitia mdomo wa uterasi, unaweza kuzitoa kwa upole kwa kidole kilichofishwa vimelea kilichovalishwa glavu. Usijaribu kufanya hadi ukamilishe mafunzo yako ya kiutendaji katika ustadi huu. Mpe mwanamke µg400 (mikrogramu) ya misoprostol kwa mdomo kabla ya kumpa rufaa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.
Utoaji mimba usiokamilika
Utoaji mimba usiokamilika ni wakati sehemu ya tishu za fetasi au plasenta zingali kwenye uterasi na seviksi imefunguka. Ukiacha utoaji mimba usiokamilika bila matibabu kwa muda, kunao ongezeko la hatari kuwa itatatizwa na maambukizi na hili linaweza kuwa tisho la maisha ya mwanamke.
Utakapo hudhuria mafunzo ya kiutendaji yanayohusiana na kipindi hiki utaona jinsi tishu iliyobaki kwa uterasi inaweza kutolewa kwa vifaa, kwa kutumia mbinu inayoitwa uhamishaji na kuretaji. Pia utajifunza jinsi ya kumpatia mwanamke dawa kwa njia ya mdomo na kumdunga sindano katika misuli ya paja au matako (udungaji wa sindano ndani ya musuli, au IM) ili kusaidia katika njia hii.
Utoaji mimba ulio hatari
Mimba ikitatizwa na uvujaji damu kutoka ukeni, lakini seviksi imefungika inaweza kuashiria utoaji wa mimba ulio hatari. Kuna uwezekano ujauzito unaweza kuendelea kwa kawaida, ikiwa fetasi inaonyesha dalili za kuishi.
 Ikiwa utashuku utoaji wa mimba ni hatari, rufaa mwanamke kwenye kituo cha afya kilichoko karibu, wanapoweza kutunza mimba.
Utoaji mimba usioepukika
Utoaji mimba usioepukika ni wakati fetasi iko kwenye uterasi, lakini ujauzito haswa utafika mwisho fetasi ikitolewa. Mara nyingi mwanamke huwa na maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio na badiliko la seviksi linaloitwa ufutaji, wakati seviksi imejivuta nyuma na kuwa nyembamba; halafu seviksi inaanza kupanuka na kufunguka kama wakati wa leba ya kawaida ya kipindi kilichokamilika. (Utajifunza kuhusu ufutaji na kupanuka kwa seviksi katika, Moduli inayofuata ya Utunzaji wa leba na kuzaa. Vilivyoko kwenye uterasi vitatoka nje pekee yake lakini ikiwa hili halitafanyika, utafunzwa umpatie mwanamke µg400 (mikrogramu) za misoprostol kwa mdomo, ikirudiwa mara moja baada ya masaa 4 ikilazimu. Usijaribu kufanya hivi hadi ukamilishe mafunzo yako katika ustadi huu.
Utoaji mimba usiofanikiwa
Wakati fetasi yote iko kwenye uterasi, lakini haina ishara zozote za kuishi na seviksi imefungika kabisa, hali hii huitwa utoaji mimba usiofanikiwa. Fetasi iliyokufa huenda ikabaki kwenye uterasi kwa muda labda itolewe katika kituo cha afya cha kipekee.
 Kutoa fetasi iliyokufa baada ya utokaji wa mimba usiofanikiwa kwa kawaida huhitaji huduma za kipekee za hospitali bora, kwa hivyo unapaswa kufanya kila juhudi za kumpa mwanamke rufaa kwenye kituo cha afya cha juu zaidi kilicho karibu.

20.2.4 Mtazamo wa kisheria kuhusu utoaji mimba

Katika nchi kadhaa, utoaji mimba umekubaliwa tu ili kuokoa maisha ya mwanamke, kulinda afya yake, na katika visa vya ubakaji. Katika nchi hizo, utoaji mimba sio makosa wakati inapofanywa ili kuokoa maisha ya mwanamke au afya yake; katika kesi za ubakaji, kujamiiana kwa maharimu au kuharibika sana kwa fetasi; au wakati mwanamke mjamzito hukosa uwezo wa kumtunza mtoto wake kwa sababu ya uchanga wake wa umri au upungufu wake wa kimwili au afya yake ya kiakili.
  • Semira amekueleza kuwa ni mjamzito. Yuko katika afya bora. Hana mtu aliye imara na hataki mtoto. Je, sheria inamruhusu kutoa mimba? Eleza ni kwa nini ndio au la.

20.2.5 Njia za kutekeleza uavyaji mimba

Utoaji mimba wa kupanga uliosalama hutekelezwa kwa kina mama wanaofikia vigezo vya sheria vilivyoelezwa hapo juu na walio tayari kutamatisha ujauzito. Taratibu hutekelezwa kwa kituo cha afya au hospitali, kwa hivyo unapaswa kuwapa rufaa wanawake wanaotafuta huduma ya kutoa mimba wazuru kituo cha juu zaidi cha afya. Njia za kuendeleza utoaji mimba wa kisheria hutegemea umri wa kipindi cha ujauzito na vifaa vinavyopatikana mahali pale. Hujumulisha:
  • Tiba ya utoaji mimba: wanawake hupewa dawa za kutekeleza utoaji wa mimba
  • Aspiresheni ya tupu uliotengezwa kwa mkono: kutumia kifaa kama sindano kinachotumiwa kwa mkono na kusababisha shinikizo la hasi ili kufyonza nje na kuvuta viliyomo katika uterasi.
  • Uhamishaji na kuretaji: kutoa vitu vilivyomo katika uterasi kwa kutumia vifaa vya chuma kutoa tishu za fetasi na kusafisha kuta za ndani za uterasi.
Kumbuka kuwa wanawake huhitaji usaidizi wa kihisia kabla, baada na wakati wa kutoa mimba uliopangwa, kama vile wanavyohitaji baada ya mimba kutoka pekee yake. Katika kitengo kifuatacho, tutaeleza huduma unazopaswa kutekeleza kwa mwanamke baada ya kutoa mimba.

20.3 Utunzaji wa mwanamke baada ya kutoa mimba

Nchi zingine katika Kusini mwa Jangwa la Sahara zina miongozo ambayo hufafanua utunzaji wa mwanamke baada ya kutoa mimba kama vile:
'Mtazamo wa kutoa huduma za utoaji mimba unaozingatia vipengele mbalimbali vinavyoathiri mahitaji ya afya ya kiakili na kimwili ya mwanamke, hali yake mwenyewe, na uwezo wake wa kupata huduma... zinazomsaidia mwanamke katika utekelezaji wa haki yake ya kijinsia na uzazi.'
(Ustadi na Utaratibu wa kutoa huduma bora za uavyaji mimba Kusini mwa Jangwa la Afrika, 2006)

20.3.1 Malengo ya huduma baada ya kutoa mimba

Malengo ya utunzaji wa mwanamke baada ya kutoa mimba ni:
  • Kutoa huduma salama, zilizo na ubora wa hali ya juu.
  • Kupeleka huduma hadi kwa watu walio vijijini iwezekanavyo.
  • Iwe rahisi na inayokubalika kwa wanawake.
  • Kuelewa hali ya kipekee ya kijamii ya kila mwanamke na mahitaji yake binafsi, na kumpatia utunzaji wake ipasavyo.
  • Kupunguza idadi ya mimba zisizopangwa na utoaji wa mimba.
  • Kutambua na kuhudumia wanawake walio na mahitaji mengine ya kijinsia au mahitaji ya kiafya ya uzazi.
  • Iwe rahisi na inayodumu katika mfumo wa afya.
Ili kutimiza malengo haya, unao wajibu wa kutekeleza, pamoja na kutambua mahitaji ya kibinafsi na hali ya jamii ya wanawake binafsi na kuwaelekeza wanapoweza kupata utunzaji unofaa katika mahali panapofaa. Unapaswa pia kuchukua hatua inayofaa kuhusu barua yoyote ya rufaa ambayo mwanamke anaweza kurudisha kijijini kutoka kwenye kituo cha ngazi ya juu zaidi cha afya.

20.3.2 Ujumbe muhimu kwa wanawake baada ya mimba kutoka pekee yake au uliopangwa

Kutoa usaidizi wa kihisia
Mchoro 20.2 Ujauzito ukifika mwisho mapema, msaidie mwanamke kupata nafuu ya kihisia.
Ujauzito unapofika mwisho mapema, mwanamke anaweza kuwa na hofu, huzuni, au mfadhaiko au anaweza kuhisi mwenye hatia au kuaibika. Wanawake wengi, hasa ambao hawajaolewa, huhisi kuwa ni lazima wafiche uharibikaji wa mimba au utoaji wa mimba uliopangwa kwa sababu ya fikira dhidi ya ngono, kupanga uzazi au utoaji mimba katika jamii zao. Kama mhudumu wa afya wa karibu zaidi na aliyeaminika sana, unao wajibu muhimu wa kutekeleza katika kumhurumia mwanamke na kumpa usaidizi wa kihisia (Mchoro 20.2).
Iwapo mimba ilitoka pekee yake, mjulishe kuwa hii hutokea mara nyingi kwa sababu ya ugonjwa wa mama au matatizo ya fetasi inayokua. Mhakikishie kuwa kuna uwezekano wa kuwa na ujauzito nzuri unaofuata, isipokuwa kama kumekuwa na maambukizi kwa uterasi, au chanzo cha kuharibika kwa mimba hakijatambuliwa na inayoathari kwa mimba inayofuata. Ikiwa mwanamke anahitaji mtoto mwingine, mshawishi acheleweshe ujauzito unaofuata mpaka apone vizuri kutokana na uharibikaji au utokaji wa mimba.
Kuvunja mfuatano wa mimba zisizohitajika
Wajibu mwingine ni kutoa huduma ya upangaji uzazi kwa wale wanaohitaji, pamoja na kuvunja mfuatano wa mimba zisizohitajika na utoaji wa mimba zilizopangwa. Ikiwa ujauzito hauhitajiki baada ya kutoa mimba na hakuna matatizo ya kudumu zinazohitaji matibabu zaidi, mwanamke anapaswa kupokea ushauri wa kutosha na usaidizi wa kuchagua njia inayofaa zaidi ya kupanga uzazi ambayo inaweza kutekelezwa moja kwa moja. Kitengo 20.5 cha kipindi hiki kinaeleza utangulizi mfupi wa upangaji uzazi baada ya kutoa mimba.
Utunzaji baada ya kutoa mimba salama
Baada ya mimba kutoka pekee yake au iliyopangwa kwa usalama, Mjulishe mwanamke atarajie kuhisi maumivu madogo au spazimu katika sehemu ya chini ya fumbatio lake, na uvujaji wa damu kidogo kutoka ukeni – sio zaidi ya damu ya hedhi ya kawaida. Mjulishe jinsi yeye na familia yake wanaweza kumtunza kwa siku chache (Mchoro 20.1).
Kisanduku 20.1 Utunzaji baada ya mimba kutolewa salama
Utunzaji bora baada ya mimba kutoka pekee yake au mimba uliopangwa unaweza kuzuia maambukizi na kusaidia mwili wa mwanamke kupona haraka. anapaswa:
  • Kunywa viowevu vingi na kula vyakula vilivyo na virutubishi.
  • Kupumzika mara kwa mara na kuepukana na kazi nzito kwa wiki.
  • Kuoga kila siku, lakini hapaswi kusafisha kaviti au kuketi kwa bafu au beseni ya maji mpaka siku chache baada ya uvujaji damu kukoma.
  • Kutumia nguo safi au pedi kushika damu yoyote, na kubadilisha pedi mara kwa mara.
  • Kutotia kitu chochote ndani ya uke, na kuepukana na ngono kwa angalau siku chache baada ya uvujaji damu kukoma.
Mwambie akujulishe mara moja au atafute usaidizi kutoka kwenye kituo cha afya cha juu ikiwa anazo ishara zozote za onyo zilizoorodheshwa katika kitengo kifuatacho.

20.3.3 Utunzaji wa kufuatilia baada ya kutoa mimba

Uzuiaji wa magonjwa yanayohusishwa na utoaji wa mimba na vifo hutegemea upatikanaji wa utunzaji wa mwanamke baada ya kutoa mimba katika mfumo wote wa utunzaji afya. Kama ni habari ya afya na elimu, uimarishaji wa dalili na utoaji rufaa wakati unaofaa, njia salama za kutoa mimba, au utunzaji wa kipekee kwa matatizo makali, angalau baadhi ya sehemu za utunzaji baada ya utoaji wa mimba unapaswa kupatikana katika kila mahali pa kutoa huduma ya uzalishaji katika mfumo wa utunzaji afya, pamoja na vituo vya afya. Ikiwa mwanamke alikuwa na uharibikaji wa mimba au utoaji mimba wa kupanga uliosalama katika kituo cha afya, anao uwezekano mdogo wa kupata maambukizi hatari au jerahi kuliko mwanamke ambaye alifanyiwa utoaji wa mimba kwa njia haramu na mtu aliyetumia vifaa visivyo salama.
Utunzaji wa dharura baada ya kutoa mimba inamaanisha hatua unazopaswa kuchukua ikiwa matatizo yaliyo katika Kisanduku 20.2 yatatokea kutokana na utoaji wa mimba.
Kisanduku 20.2 Matatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyosalama
Tatizo kuu la hatari zaidi ni kifo. Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya vifo vya kina mama ni kwa sababu ya utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama. Kwa kila mwanamke anayekufa, imekadiriwa kuwa wanawake wengine 16 hadi 33 huwa na tatizo baada ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama, pamoja na:
  • Hemoreji (kutokwa na damu nyingi)
  • Maambukizi katika kaviti ya pelvisi, au katika mkondo wa damu. (kwa mfano, pepopunda)
  • Kutoboka kwa uterasi (kushona mraruko wa kuta za uterasi kwa kifaa kilicho na ncha kali.
  • Jerahi lililokaribu na ogani katika kaviti ya pelvisi (kwa mfano, uke, kibofu cha mkojo, rektamu na utumbo)
  • Sumu kutokana na dozi ya dawa iliyozidi kipimo chake au mitishamba inayotumiwa kutekeleza utoaji mimba wa kupanga.
Hapo baadaye, mwanamke anaweza kuugua kutokana na maumivu ya pelvisi yanayoendelea kwa muda mrefu (yanayojirudia), hasa wakati wa hedhi, mimba kutoka pekee yake unaojirudia au utasa.
 Ikiwa mwanamke anayo ishara yoyote kati ya hizi baada ya kutoa mimba, mwelekeze kwenye kituo cha afya kilichoko karibu au hospitali
Unapaswa kuchunguza afya ya mwanamke, mpigo wa mshipa, halijoto, shinikizo la damu mara kwa mara baada ya kutoa mimba na mwulize na uwe makini ikiwa anayo ishara na dalili zinazofuata:
  • Maumivu makali ya spazimu katika sehemu ya chini ya fumbatio.
  • Sehemu ya chini ya fumbatio lililovimba au lililongumu bila sauti au mibubujiko ndani.
  • Uvujaji wa damu nzito, donge kubwa la damu au kuvuja damu kwa zaidi ya wiki 2
  • Harufu mbaya kutoka ukeni.
  • Joto jingi mwilini: halijoto ya sentigredi 38 au iliyo juu.
  • Mpigo wa kasi wa mshipa: zaidi ya mipigo 100 kwa dakika.
  • Kuhisi kichefuchefu sana, kupoteza fahamu, au kuwa na kizunguzungu.
  • Shinikizo la damu lililochini au linaloshuka, chini ya kiwango cha kawaida ya mmHg 120/70.
Ikiwa kutatokea uvujaji wa damu nzito, unaweza kushindwa kuona kama damu inavuja kwenye fumbatio lake kutoka kwenye jerahi au ogani nyingine ya ndani, ambalo linaweza kutendeka baada ya kutoa mimba. Upotezaji wa damu nyingi unasababisha hali inayoitwa mshtuko (Kisanduku 20.3).
Kisanduku 20.3 Ishara za mshtuko
Mwanamke aliye na mshtuko ataonekena mwenye rangi ya buluu hafifu na kutokwa na jasho, na mpigo wa kasi wa mshipa (juu ya mipigo 100 kwa kila dakika), upumuaji wa kasi, shinikizo la damu lililo chini au linaloshuka (shinikizo la diastoli – nambari ya chini - iko chini yammHg 60), na kizunguzungu au kuchanganyiwa; anaweza hata kupoteza fahamu. Ni lazima uchukue hatua mara moja ili kuokoa maisha yake.

20.3.4 Matibabu ya rufaa ya awali katika dharura

Matibabu ya dharura ya wagonjwa walio katika mshtuko ni pamoja na kuanzisha utiliaji dawa mishipani, yaani kupeleka kiowevu kilichofishwa vijidudu kinachoitwa Salini ya kawaida au kiowevu cha unyonyeshaji cha Ringer, moja kwa moja ndani ya mshipa ili kuchukua nafasi ya viowevu vya damu na chumvi ambavyo vinapotezwa kupitia uvujaji wa damu nzito. Utajifunza nadharia ya jinsi ya kufanya hivi katika Kipindi cha 22 cha Moduli hii, na katika mafunzo yako ya utendaji. Mara tu utiliaji wa dawa mishipani unapokuwa tayari, lazima upeane rufaa ya dharura ya wanawake kwenye kituo cha afya kilicho karibu
Mchoro 20.3 Mlalishe hivi mwanamke anayevuja damu na umsaidie haraka kupata utunzaji wa dharura.
Wakati wa kumsafirisha, hakikisha kuwa umemlalisha anavyofaa na kichwa chake kikiwa mahali palipo tambarare ( usitumie mto) na miguu yake ikiwa imeinuliwa na kuegemezwa (tazama Mchoro 20.3). Hali hii husaidia shinikizo lake la damu kutoshuka zaidi. Ikiwezekana, unapaswa kuandamana naye hadi kituo cha afya ili kuendeleza utiliaji wa damu kwenye mishipa na mfuko wa kiowevu cha IV kikishikiliwa juu yake. Ikiwa huwezi kwenda naye, eleza atakayeandamana naye umuhimu wa kumweka mama na mfuko katika mahali paliposhauriwa; Pia mjulishe jinsi ya kufunga tyubu wakati kiowevu kimeisha katika mfuko wake. Kwa kawaida, tuma mtu mwenye afya andamane naye anayeweza kutolea damu ikiwa atahitaji kuongezwa damu afikapo kituo cha afya.
Hakikisha kuwa umeandika barua ya rufaa
  • Je, unakumbuka maelezo haya? (ulijifunza haya katika Kipindi cha 13).

20.4 Visababishi vingine vya kuvuja damu mapema wakati wa mimba

Dalili za hatari na matibabu ya dharura yaliyoelezwa hapo juu zinahusiana na visababishi vingine viwili vya kawaida vya kuvuja damu mapema wakati wa ujauzito.

20.4.1 Mimba iliyotungika nje ya uterasi

 Iwapo utashuku mimba isiyo kuwa katika sehemu yake lazima umtume mjamzito ili afanyiwe utathmini na kutibiwa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu.
Mimba iliyotungwa nje ya uterasi ni wakati mimba huwa nje ya nafasi katika emdometria ya uterasi. Eneo la kawaida zaidi ya mimba isiyo kuwa katika sehemu yake ni neli ya falopio (jozi za neli zinazoshikanisha uterasi na undani wa fumbatio, kila moja kuishia karibu na ovari kwa upande huo. Tazama nyuma kwa Michoro ya 3.3 na 5.3 kwenye Utunzaji katika Ujauzito, Sehemu ya 1, ili kujikumbusha anatomi ya uterasi na viungo vilivyokaribu. Uwezekano wa sehemu zingine ni tishu unganishi za ovari, ovari, na nafasi katika fumbatio iliyozunguka uterasi.
Ikiwa embrio itajikolea katika neva ya falopio, haitaweza kushikilia fetasi inayoendelea kuwa zaidi ya wiki chache za kwanza. Kuna uwezekano wa hatari kwamba neva itapasuka na mwanamke ataanza kuvuja damu ndani ya fumbatio. Hii ni hali ya kuhatarisha maisha inayosababisha mshtuko, ambayo ni lazima itibiwe kwa haraka ili kukomesha uvujaji wa damu. Dalili za kawaida za mimba isiyokuwa katika sehemu yake ni maumivu ya sehemu ya chini ya fumbatio, hedhi iliyochelewa, na kuvuja damu ukeni au kwa undani.

20.4.2 Mimba isiyokuwa ya kawaida

Kila utakapo shuku mimba isiyokuwa ya kawaida, lazima umpeleke mama kwenye kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Sababu nyingine ya kuvuja damu mapema wakati wa ujauzito ni mimba isiyokuwa ya kawaida, ambayo ulijifunza katika Kipindi cha 10. Unaweza kupatana na tatizo hili mara kwa mara. Ina dalili ya ukuaji usiokuwa wa kawaida wa tyuma ulioundwa kutokana na plasenta ya baadaye mapema wakati wa awamu ya kwanza ya mimba. Uterasi hujazwa na tishu iliyoonekana kama zabibu na kuwa kubwa kuliko ukubwa utakaofikia kwa hatua kamili ya mimba ya kawaida (Mchoro 20.4).
Mchoro 20.4 Mimba isiyokuwa ya kawaida (tyuma) ina kuwa kwa uterasi badala ya mtoto.
  • Je, unaweza kukumbuka dalili za mimba isiyokuwa ya kawaida?
Mojawapo ya matatizo yanayoogopesha katika mimba isiyokuwa ya kawaida ni kunaweza kusababisha utokaji wa damu nyingi na kuweza kusabisha kifo cha mama. Ikiwa mama atakuwa anatokwa na damu ukeni, anza kwa kutia viowevu ndani ya mshipa (kama ilivyoelezwa katika Kipindi cha 22 na mazoezi katika vitendo vyako vya ujuzi) kabla ya kumpa rufaa. Kiowevu kinapaswa kutiririka matone 60 kwa dakika. Mama anapaswa kupelekwa katika kituo cha afya na watu wazima wenye afya ambao wanaweza kumtolea damu.

20.5 Upangaji uzazi baada kutoa mimba

Katika sehemu ya mwisho ya kipindi hiki, tunaingia kwa haja ya kupanga uzazi baada ya kutoa mimba. Katika matukio mengi, utoaji wa huduma ya dharura baada ya kutoa mimba unaweza kuwa mojawapo ya matukio ambayo mama na mpenzi wake uwasiliana nayo na mfumo wa huduma ya afya. Hivyo basi, inawakilisha fursa muhimu kwa kutoa taarifa na huduma ya upangaji uzazi.
Upangaji uzazi baada ya kutoa mimba inapaswa kuwa ni pamoja na vijenzi vifuatavyo:
  • Kushauri kuhusu mahitaji ya kupanga uzazi kulingana na malengo ya uzazi wa mteja
  • Maelezo na ushauri kuhusu njia zote zilizopo, sifa zao, zenye kuleta matokeo yanayotarajiwa, na madhara (tazama mchoro 20.5)
  • Uchaguzi kati ya utaratibu (kwa mfano, wa muda mfupi na wa muda mrefu, yenye homoni, na isiyo na homoni)
  • Kuhakikisha kwamba unaendelea kutoa upangaji uzazi, ili mama asiishiwe na ulinzi:
    • Kupatikana kwa huduma ya kufuatilia
    • Taarifa kuhusu mahitaji ya kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.
Mchoro 20.5 Baadhi ya mbinu za kuzuia mimba.
Upangaji uzazi baada ya kutoa mimba pia inapaswa kuzingatia utathmini wa mtu binafsi kwa kila hali ya mwanamke: tabia yake binafsi, hali ya kliniki, na uwezo wa utoaji huduma katika jamii ambako anaishi. Utajifunza kuhusu haya yote kwa undani katika Moduli ya Upangaji Uzazi katika mtaala huu. Wanawake wengi watapata upangaji uzazi baada ya kutoa mimba wakiwa katika kituo cha afya cha ngazi ya juu, lakini wachache wanaweza kuwa wametoka mapema. Unaweza pia kuhitajika kuendelea kuwapa mbinu za kuzuia mimba wakiwa katika jamii yako. Hivyo hii ni eneo moja unajukumu kubwa kwa utoaji wa huduma kwa wanawake waliotoa mimba.

20.5.1 Wakati wa kuanza upangaji uzazi

Huduma ya upangaji uzazi baada ya kutoa mimba inapaswa kutekelezwa mara moja, kwa sababu uwezo wa kupata mimba hurudi haraka: katika wiki mbili baada ya kutoa mimba au kuharibika kwa mimba katika awamu ya kwanza, na utoaji wa mimba au kuharibika kwa mimba katika wiki ya nne baada ya awamu ya pili. Wanawake wote wanaopokea huduma baada ya kutoa mimba wanahitaji ushauri na habari kuhakikisha wataelewa kuwa wanaweza kupata mimba tena kabla ya awamu ya kwanza ya hedhi, na kwamba kuna mbinu salama za kuzuia mimba au kuchelewesha mimba.
Ikiwa mwanamke anataka kupata mimba tena hivi karibuni, mshawishi angoje. Miezi sita baada ya mimba kutoka pekee yake au kutoa mimba uliopangwa kuna uwezekano wa kuzaa mtoto aliye na uzito mdogo au mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake na mama kupata anemia.
Katika kipindi kifuatacho, utaongezea kile umejifunza katika kipindi hiki tutakapoeleza sababu za kuvuja damu katika awamu ya mwisho ya ujauzito na namna ya kudhibiti hali hii ya dharura.


Muhtasari wa Kipindi cha 20

Katika Kipindi cha 20, umejifunza kwamba:
  1. Kuvuja damu mapema wakati wa uajuzito hutokea kabla ya wiki 28 ya mimba.
  2. Utokaji wa mimba pekee yake (kuharibika kwa mimba) hutokea kwa takriban mimba 15%.
  3. Visababishi vya kawaida vya uvujaji wa damu mapema wakati wa ujauzito ni utoaji wa mimba uliopangwa au mimba kutoka pekee yake, mimba isiyokuwa katika sehemu yake, na isiyokuwa ya kawaida. Hali hizi zinaweza kusababisha matatizo makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya wajawazito, hasa wakati mtu asiyekuwa na ujuzi atatoa mimba kwa njia isiyo kuwa salama katika mazingira ma machafu.
  4. Ruhusa ikitolewa, wanawake wanaweza kupata huduma za utoaji wa mimba uliosalama katika vituo vya afya. Matibabu na Upasuaji zipo zakuuchagua huduma ya kutoa mimba kwa njia iliyosalama ukizingatia sheria.
  5. Dalili hatari baada ya kutoa mimba ni pamoja na uchungu mkali wa spazimu katika sehemu ya chini ya fumbatio, fumbatio uliovimba au ulio mgumu, kuvuja damu nyingi, harufu mbaya kutoka ukeni, joto jingi mwilini, mdundo wa haraka katika mshipa, kichefuchefu, kizunguzungu na mshtuko. Hizi ni dalili kwamba matibabu ya dharura na rufaa zinapaswa kuanza mara moja.
  6. Matibabu ya dharura ya kuvuja damu au mshtuko ni pamoja na kutilia dawa kwa mshipa kabla ya kumpeleka mama kwenye kituo cha afya, akiandamana na mtu anayeweza kumpatia damu.
  7. Upangaji uzazi inapaswa kuwa nzuri kwa mwanamke baada ya huduma ya kutoa mimba, ili kuvunja anuai katika hali ya utoaji wa mimba uliopangwa na kumpatia muda wa kupata nafuu katika hali ambazo mimba ilitoka pekee yake.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri