Idadi ya wagonjwa wa corona nchini Kenya yafikia 1,214 baada ya kutangazwa wagonjwa wapya 22

Wagonjwa wapya 22 wa corona wamethibitishwa KenyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWagonjwa wapya 22 wa corona wamethibitishwa Kenya
Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona Kenya imefikia 1,214, baada ya wagonjwa wapya 22 kuthibitishwa siku ya Jumapili.
Wakati wa mkutano na vyombo vya habari , katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kwamba wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 24 hadi 73 ,huku, wanaume wakiwa 17 na wanawake wakiwa watano.
Akitoa habari njema , Dkt Aman amesema kwamba wagonjwa watatu waliondoka hospitalini na hivyo basi kufanya idadi ya wagonjwa waliopona virusi hivyo kufikia 383.
Amesema kwamba mgonjwa mmoja ambaye aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika eneo la Mathare alifariki, na kufanya idadi ya waliokufa nchini humo kufikia watu 51.
Amesema kwamba idadi ya watu waliopimwa virusi hivyo kufikia sasa ni 59,260.
Amesema kwamba wagonjwa 10 wanatoka katika mji wa Nairobi, 9 wanatoka Mombasa, mmoja anatoka Kwale na Nakuru na Taita taveta yakiwa na mgonjwa mmoja mmoja.
Aman amewataka Wakenya kuendelea kufuata maagizo ya serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema kwamba masharti hayo ni muhimu na huenda yakaimarishwa katika maeneo kadhaa ya nchi iwapo maambukizi yatazidi kuongezeka.
Amewapongeza wakazi wanaoishi katika mitaa iliowekewa amri ya kutotoka nje kwa saa 24 kwa kufuata maagizo ya serikali.Aliwasihi wakenya kujitokeza kwa wingi ili kupimwa.
Coronavirus
Hatua iliyochukuliwa na Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta alitangaza mipango ya kusaidia biashara na raia kusonga mbele katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi kwasababu ya janga la virusi vya corona
Rais alihutubia taifa kutoka Ikulu ya rais, Nairobi na kusema kwamba mipango hiyo itagharimu shilingi bilioni 53.7.
Katika hotuba yake, rais alisema pesa hizo zitagawanywa katika sekta muhimu kama vile miundo mbinu, elimu, biashara ndogo ndogo na za wastani, afya, kilimo, utalii, mazingira na viwanda vya uzalishaji.
Aidha, rais amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.
''Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia zimeanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, musiende makazi, namna hio. Lakini, ile kitu ambayo itatusaidia pia kwa kikamilifu kuhakikisha ya kwamba tumeweza tena kufungua uchumi wetu na wananchi waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida. Nimewaambia wenzangu, hii haitakuwa kwa sababu ya yale serikali itatenda, itakuwa kwa sababu ya yale kila mmoja wetu kwa kibinafsi atafanya''.
Kenya inachukua hatua sawa na zile ambazo pia zimechukuliwa na nchi nyengine kama hatua ya kuuinua uchumi unaoendelea kudidimia.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri