KINA MAMA ACHENI KUTOA MIMBA KWA MAKUSUDI SOMA KISA CHA MAMA HUYU Martha Anne-Bowre mwanamke anayejuta kuavya mimba 5 kwa makusudi

Mama Martha Anne-BowreHaki miliki ya pichaMAMA MARTHA ANNE-BOWRE
Uavyaji (utoaji) mimba ni kinyume cha sheria katika baadhi ya mataifa barani Afrika jambo ambalo limekuwa likichangia wasichana na hata wanawake kutafuta njia za siri na ambazo ni hatari kulitekeleza hilo.
Martha Anne Bwore mwanaharakati anayepinga uavyaji mimba nchini Kenya aliye na miaka 55 anaeleza namna hofu na mahangaiko wanayopitia wasichana wakati wanapoachwa bila mawaidha au muongozi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na tendo la ndoa vinavyopelekea uavyaji mimba.
Na ni jambo ambalo analifahamu kwa uzito wake, kutokana na kuipitia hali kama hiyo na kuishia kuavya sio mimba moja wala mbili, lakini sita. Japo kati ya hizo mimba moja ilibidi atolewe ili kuokoa maisha yake.
Kilichomshinikiza, anaeleza ni matamanio ya kupata mpenzi wa kuishi naye, kwani wapenzi aliobahatika kuwa nao walimshinikiza kuavya mimba ili kuendeleza mahusiano hayo.

Uhuru wa maisha kwa mara ya kwanza

uavyaji mimba haramu AfrikaHaki miliki ya pichaGIANLUIGI GUERCIA
Bi Martha anasema alilelewa na wazazi waliokuwa wakali ambao hawakumruhusu hata kutoka nje.
Suala la ngono au mahusiano ni mambo ambayo yalikuwa mwiko kujadiliwa katika familia yake.
Uhuru wa maisha aliuonja kwa mara ya kwanza nchini India alikokwenda kusoma akiwa na umri wa miaka 17.
Hapakuwa na mzazi wala mlezi yeyote aliyekuwa akimfuatilia tabia zake.
"Nikiwa India nilikuwa na hela, pombe, wapenzi na uhuru. Kisha hakukuwa na wingi wa warembo kwa hio tulichukuliwa kama malkia ," alisema Bwore .
Ni katika mapito hayo ya maisha ndipo Martha aligundua kuwa alikuwa mja mzito kwa mara ya kwanza.
Kutokana na shinikizo la masomo aliamua pamoja na mpenziwe wakati huo kuiavya mimba.
India ni mojawapo ya nchi ambazo zinasheria inayoruhuhusu uavyaji mimba.
Haikuchukua muda kabla ya Bwore kuendelea na maisha yake ya anasa na muda sio muda akapata ujauzito mwengine.
Martha Anne-Bowre akihadithia yaliomsibu katika BBC Swahili
Image captionMartha Anne-Bowre akihadithia yaliomsibu katika BBC Swahili
"Nilipomwambia mpenzi wangu kuwa nimeshika mimba alisema kuwa niiavye kwa kuwa tulikuwa bado vijana. Mimi ni yule mtu nikipenda naweza kufanya chochote kwa hivyo niliamua kuavya ."
Lakini haikuchukua muda kwa yeye kupata mimba kwa mara mara ya tatu lakini hio ilitunga kwenye mirija ya njia ya mayai ya mwanamke na hivyo kutakiwa kutolewa ama la ingehatarisha maisha yake.
Baada ya mimba hiyo ya tatu, alianza kuwa na msongo wa mawazo na hapo alikunywa pombe kwa wingi na pia kujihusisha zaidi na ngono akiamini ndio njia ya kuyaondoa mawazo.
Miaka miwili baadaye "nilishika mimba ya nne".
Mpenzi wake wakati huo alimshurutisha aavye mimba hiyo licha ya kuwa yeye alitaka iwe siri ili awe mama. Lakini mpenzi wake alipogundua ilimbidi aitoe.

Pacha walioibadili roho

Mama Martha Anne-BowreHaki miliki ya pichaMAMA MARTHA ANNE-BOWRE
Image captionMama Martha Anne-Bowre: Mwanamke anayejuta kuavya mimba 7 kwa makusudi
Martha anasema alipata mpenzi mwengine akiwa India na haikuchukua muda kabla yeye kushika mimba. Kama ilivyokuwa ya wapenzi wake wa awali, hata huyu alimshurutisha aavye mimba.
"Hii mimba ilikuwa ya miezi 5. Nilimweleza daktari kuwa nilitaka kuavya mimba, lakini daktari alinishauri nipigwe picha ya mimba kabla ya kuitoa na hapo iligundulika nilikuwa nimebeba mapacha ."
"Baada ya siku mbili za uchungu kupitia sindano nilizodungwa ili mimba itoke kwa uchungu niliwatizama mapacha wangu mvulana na msichana wakiwa wamekumbatiana baada ya kutoka, nililia saana na kumuomba Mungu msamaha na hapo niliapa kutotoa mimba tena," Bwore alisema .
Haikuchukuwa muda kabla ya yeye kushika mimba nyengine lakini wakati huu aliamua kuwa angezaa mtoto iwe atakuwa na mpenzi au la.
Marie Stopes yazuia huduma za uavyaji wa mimba Kenya
Matokeo ni kuwa Bwore ana watoto wawili, msichana mwenye umri wa miaka 27 hii leo aliyemzaa akiwa bado masomoni huko India na Mvulana aliye na miaka 21 aliyemzaa baada ya kurejea nchini Kenya.
Kwa sasa Bwore ni mmoja wa watu wanaopinga uavyaji mimba.
Anajishughulisha kutoa ushauri kwa wasichana ambao wamefika mwisho na wanaotamani kutoa mimba hadi wakati ambapo wana imarika kimawazo.
Japo anajutia saana msururu wa mimba alizozitoa, anapania kutumia hali yake kama njia ya kuhamasisha umma dhidi ya hali hii ambayo inasema haifai.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri