WANDOTO WANGU!!!! MWANDISHI: MAKUMPILA THE DON.



 Kwa uzuri wako  na tabianzako zilizo nikosha nilikufanya mwanamke wa maisha yangu yote sikutizama nyuma tena nikaacha tamaa zote za dunia nikaamua kuishi nawe wala sikutamani wadada wengine wenye sifa na maumbo mazuri. Nikakupenda wewe cheusi wangu. Nikaapa mbele ya kanisa na binadamu kuwa we ndiye fungu langu mama wa wanangu mbeba thamani yangu, uliye nafasi yangu nikakufanya wa ndoto wangu.

(UMENITENDA HAYA?)

Naitwa Nelson tangu nikiwa mtoto mama alinionya sana kuhusu wanawake ikiwa nae ni mwanamke kama wao hao alionikanya, kuwa  hawaeleweki na hawajawahi jua kipi wanataka katika maisha kwani, ukimsifia unampata, ukimhudumia mahitaji yake unampata, ukimuowa masikini akikutana na tajiri basi hutomuona, ukiwa napesa usipo mridhisha kitandani atamtafuta hata muuza karanga ili tu akatimiziwe haja yake. Na huyo ndiye atakae muheshimu na kumtii sana kuliko wewe ulimuweka ndani.

Nimepita katika ngazi zote za shule na sasa npo chuo kikuu lani hapa nchini, nikuchukua fakati ya uhasibu, nilipo ingia mwaka wa kwanza sikujua kuwa chuo ni dunia nyngine ya maisha tofauti na tulinayo = ,maisha ya kifahari hata kwa asiye kuwa nacho kwani hufeki maisha wadada wasio na hata maisha mazuri kwao wao pia hujifanya wana maisha mazuri kwa kutafuta madanga mjini ili tuwaonao wawe kama wale ambao ,maisha yao yako poa. Nilianza mwaka wa kwanza katika hali ya kawaida nguzo yangu kuu ilikuwa ni kusoma kwa bidii zote na kukaza buti haswaa kwani ndiyo alikuwa msaada wangu m wanaisha yajayo mbele yangu, nili soma kwa bidii huku nikizingatia sana maneno ya mama angu kuwa huna urithi ntakaokupa mwanangu zaidi ya elimu ntakayo kuachia kichwani mwako zingatia sana elimu, niliyaandika kwenye kila daftari nililo nunua jipya kwenye jarada gumu mwanzo tu mwa daftari. Mwaka wa kwanza umepita tuko mwaka wa pili tukitoka likizo, hapo sasa ndipo mambo yalipo anza kubadirika kwani nilikutana na binti wa mwaka wakwanza kama ujuavyo hakuna mkate mgumu mbele ya chai nikanasa. Twende sasa………..

Binti huyu alinifata siku ya kwanza nikiwa nimekaa darasani najisomea akitakanimeulekeze ofisini kwan alikuwa mgeni wa chuoni pale na majengo ni mengi hivyo hakujua wapi aanzie make ndo alikuwa analipoti chuoni pale. Nilimsikilza,

“kaka samahani”

, kuinua macho alikuwa malaika kashuka mbele angu duu!! Mtoto mzuri cheusi nikaduwaa duwaa kidogo……..

“yes bila samahani,”

“ Je waweza nielekeza ilipo administration??”

 Sikumjibu kitu, “nikamuliiza dada hivi kwenu husalimiagi watu ukiamaka tu unakurupuka na kwenda shughuri zako bila hata salamu?”

“ Ooh kaka samaahni sana, mambo?”

 Poa!! Vipi?

“Samahani waweza nielekeza kama nilivyo kuuliza mi ni mgeni hapa sasa sijui naanzia wapi hata make majengo ni mengi hapa tafadhari nisaidie kunielekeza”

 Nikainuka nikafunga daftari zangu kimya kimya. Kisha nikamwambia nifuate akawa ananifuta kwa nyuma nyuma nipo kimya tu sizungumzi kitu nae tulipokaribia na ofisi akanishika mkono

“kaka samahani nimekuudhi kwani?”

“ Hapana hujaniudhi kwani vipi?”

 “Aah aah!! Make naona tangu tumeanz safari hatujazungumza kitu”

 “we siumetaka ofisi au?” “

“Ndiyo;

“Aya twende ofisini”

. Akakaa kimya, tukafika ofisi nikamuonyesha ilipo adminisfration, nikamsontea “

ni pale kagonge ule mlango” akajibu asante kaka kwa msaada wako”

 nikajibu

“Poa kawaida tu”

 “Poa baadae basi”

“Poa”

 Nikarudi darasani kuendelea na kazi zangu, ilipita wiki moja bila kukumbuka kilichotokea 

Akati natembea kwenye valanda ya chuoni pale nikiwa katika msongo mkubwa wa mawazo wala sikusikia kama naitwa nyuma ghafra nilisituka niliposhikwa begani na mtu nisie mjua. Nikageuka nyuma,

“ oooh kaka  samahani naona upona mawazo mengi sana make nimekuita tangu kule mbali ila hukusikia”

“ Daah samahani sana sijasikia ukiniita, mhuu nambie sasa za siku?”

“ Aah njema sana sijui wewe unaendeleaje na hali?”

“ Mi niko poa. Nambie ulifanikiwa kumaliza usajili wako vizuri?”

 Ndiyo nilipomaliza vyema asante sana kaka kwa ,msaada wako make niliwafuata makaka wawili siku ile wanielekeze wakawa waniangalia tu, ila wewe ulitoa muda wako kwa ajili angu ukafunga daftari ukanielekeza hadi ofisini. Inaonekana una roho nzuri sana eti?”

 “Hapana maigizo tu dada wala sina roho kama unayo idhania”

,” hapana kama ungekuwa na roho mbaya wala usinge nielekeza hadi ofisi na kunipeleke pia.

“ Hapana nami akati nakuja hapa nilipelekwa so kile kitendo nami nimetenda bila kujua kwanini nilitenda kwani, sifanyagi hivyo kwadada yeyote anaekuja kutaka msaada kwangu wa namna hiyo”

 “Duuh basi mi ninabahati ya pekee kusindikizwa nawe”  “Ok, usijali; Nilikuwa naelekea darasi ko ka vipi baadae sawa?” “Ooh sawa,”

 Akati napiga hatua mbele nikasikia,

 “oooh lakini kaka hii ni mara ya pili kukutana nawe naweza jua jina lako ili nisiwe nakwita majina kama wewe kaka. Namengine?”

 “Nikajibu we niite tu hayo mengine nitaitika”

“ aaah hapana mi naitwa Lightness”, “

“ooh sawa light”

 “Mmmmmmh mi naitwa Nelson, ila si Mandela wa south africa mi ni wabongo hapa hapa”

“.oky sawa baadae, au kunalingine make nachelewa pindi”

 Akacheka “ok sawa ila jina lako zuri sana”,

 hata lako pia tena lako ndo zuri sana. Ok baadae sasa eti?

“Sawa”

Nikaenda darasani huku nyuma alibaki akiwa ananitzama tuu bila kubandua macho yake kwangu, kwa tabasamu taamuu usoni mwake, nilipofika mlaongni pa darasa nikageuka nyuma nakuta bdo yu name tu kisha akapunga mkono kwa kuniaga nami sikufanya hiana nikampungia mkono kwa kumuaga pia.

Comments

Popular posts from this blog

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri