IJUE ASILI YA JUMAPILI NA IBADA YA JUA

Karibu kwa mwendelezo wetu 
tulipo ishia kwa makala iliyo pita 
Sasa endelea

VII. UFALME WA MILELE WA KRISTO (MAREJEO YAKE HADI MILELE)
Ufalme huo unawakilishwa na Jiwe lililochongwa bila kazi ya mikono
(Dan.2:34,35,44,45). Jiwe hilo ni Kristo (Luka 20:17,18; Mt. 21:42,44; Mdo. 4:10-12).
KATIKA UTAWLW HUU WA NNE ULIOANZA KUTAWALA DUNIA NZIMA RASMI MWAKA 168 kabla ya kuzaliwa kwa  KRISTO ibada za kuabudu jua , sanamu mbalimbali, ziliendelea  pamoja na sikuu mbalimbali kama vile ester na chrismaspia zilendelea. kama hizo hapo chini
Image result for rite of sun worshipingImage result for rite of sun worshiping
MIUNGU WA WAKIRUMI WA ZAMANI KABLA YESU HAJAZALIWA


Image result for rite of sun worshipingImage result for rite of sun worshipingImage result for sun god worship in india
KIPINDI CHA YESU CHOTE AKIWEPO HAPA DUNIANI HAKUWEZA KUABUDU SIKU YA JUA  HII NIKWASABABU KATIKA AMRI ZOTE KUMI ZA MUNGU HAKUNA SEHEMU ILIYORUHUSU WATU KUABUDU SIKU YA JUA YAANI SUN-DAY.
 ISIPOKUWA  ALIENDELEA KUABUDU SIKU YA SABA YAANI JUMAMOSI SOMA    LUKA 4:16
ISAYA 66: 
WAEBRANIA4:9-10
MARKO2:27-28
UFUNUO 12;14

Hata katika nchi mpya Sabato ya siku ya saba iliyobarikiwa itaendelea kutunzwa na mataifa
ya wale waliookolewa. "Na itakuwa ... Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu
mbele zangu, asema BWANA" Isaya 66:23).
Sababuk wa nini Mungu aliwaamuru wanadamu kuitunza siku ya Sabato ni hii: "Maana,
kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku
ya sabato akaitakasa" (Kutoka 20:ll).

Kwa hiyo, Sabato ni kumbukumbu ya uumbaji wa nchi hii kwa siku sita, naye Mungu
ameiweka kama ishara ya uweza Wake wa Uumbaji. Kwa njia ya kuitunza Mungu alikusudia
kwamba mwanadamu angemkumbuka Yeye daima kama Mungu wa kweli na wa pekee,
Muumbaji wa vitu vyote.

ISHARA YA UTAKASO
Uweza wa Mungu wa uumbaji ulitumika kwa mara ya pili katika kazi yake ya ukombozi,
ambayo kwa kweli ni uumbaji mpya. Sabato kama kumbukumbu ya uweza wa uumbaji
inakuwa kumbukumbu ya wokovu wetu katika Kristo. Iliwekwa dhahiri kama ishara ya
utakaso. "Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya Mimi na wao, wapate kujua ya kuwa
Mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye" (Ezekieli 20:l2).


Kuitakasa Sabato ni kuitumia kwa kusudi lile lile iliyowekewa. Ilikusudiwa kuwa siku ya
ibada kwa wote pamoja na maombi ya faragha. "Siku ya saba ni sabato ya kustarehe kabisa,

KUSANYIKO TAKATIFU" (Mambo ya Walawi 23:3). Tunacho kielelezo cha Yesu
Mwenyewe akihudhuria ibada siku ya Sabato: "Na siku ya sabato akaingia katika sinagogi
kama ilivyokuwa desturi Yake" (Luka 4:l6).

Maandalio ya kuitunza vizuri Sabato ni pamoja na kupika chakula na kuandaa vitu vingine
vinavyoweza kuhitajika ili kuwa tayari kuacha kufanya kazi za kawaida, za kidunia wakati
Sabato inapoanza, na kuutumia muda wetu kwa mambo matakatifu, ya mbinguni (Kutoka
l6:22,23; Luka 23:54).

Sabato sio siku ya kufanya kazi za kawaida, wala uzembe, wala burudani. Ni kwa ajili ya
kupumzika, kiroho na kimwili; kwa ajili ya kutafakari; ibada ya faragha na ya wote; kwa ajili
ya furaha takatifu, na kwa kusaidiana. Ilikusudiwa kuwa siku ya furaha, uchangamfu, na bora
kuliko zote katika zile siku saba.

TAHADHARI  KWA WASOMAJI WA BIBLIA, WATU WENGI HUPOTOSHWA NA SHETANI KUPITIA EIZA KUJISOMEA WAO WENYEWE AU KUPITIA VIONGOZI WAO WA KIROHO JUU YA  VITABU VYA PAUL KUHUSU AMRI KUMI ZA MUNGU NA SABATO
WAPENDWA MUNGU SI KIGEGEU HATA AJIPINGE ALIYSEMA  KUPTIA AGANO LA KALE JUU YA AMRI KUMI I ZA MUNGU NDIYE ALIYESEMA KATIKA AGANO JIPYA JUU YA  HIZO HIZO KUMI SOMA  ISAYA 46 :9YOTE

MAELEZO YAFUTAYO YANAELEZEA JUU YA MAANA YA PAUL KUHUSU SABATO



SABATO ZA KIVULI [MAADHIMISHO] ZILIKOMA
Inadhaniwa na wengine kwamba Paulo alikuwa anataja badiliko la Sabato wakati
alipowaandikia Wakolosai: "Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa
sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo
yajayo; bali mwili ni wa Kristo" (Wakolosai 2:16,17).

Mfumo wa kafara [dhabihu] (ceremonial system) wa Agano la Kale ulikuwa na sikukuu
nyingi, siku takatifu nyingi, na sabato za kila mwaka. Mfumo ule ulio"amriwa hata wakati wa
matengenezo mapya" (Waebrania 9:10), ulikufa pamoja na Kristo [pale msalabani], ambaye
huo ulikuwa ni kivuli chake. Kwa sababu hiyo, yule aliyemwamini Kristo hakulazimika
kuirudia mifano (types) hiyo na vivuli (shadows) vyake. Hakuwa na haja ya kuzishika sabato
zake saba zilizotokea kila mwaka (Mambo ya Walawi 23:4,24,32,39), [Sabato 7 za kivuli ni
hizi: l. f.7; 2. f.8; 3. f.l6,21; 4. f.24,25; 5. f.3l-32; 6. f.34,35,39; 7. f.36] zote hizo zilitakiwa
kushikwa kama nyongeza kwa au "kando ya Sabato za BWANA" (Mambo ya Walawi 23:38).
Na kama vile kafara na kawaida hizo za dini zilizoadhimishwa zilivyokuwa hazina nguvu tena,
ndivyo Mkristo muumini, katika kifungu hiki cha Wakolosai anavyotahadharishwa asije
akamruhusu mtu ye yote kumhukumu katika mambo hayo. Kifungu hicho hakina uhusiano
kabisa na Sabato ya Bwana ya siku ya saba.

Labda jambo hili litapokewa kwa upesi, na kuonekana wazi zaidi, kama mawazo yetu
yataelekezwa kwenye ufafanuzi wa kifungu hiki uliotolewa na watu maarufu wenye mamlaka.
Dkt. Adam Clarke, katika kitabu chake cha Ufafanuzi (Commentary) [Komentari]
kilichoandikwa kwa jina lake, anasema hivi kuhusu Wakolosai 2:l6:
"Hakuna taarifa hapa isemayo kwamba SABATO iliondolewa, au kwamba matumizi yake
ya kimaadili yalibatilishwa kwa kule kuanzishwa kwa Ukristo. Nimeonyesha mahali pengine
kwamba, 'Ikumbuke siku ya sabato uitakase' ni amri ya UWAJIBIKAJI UNAODUMU
MILELE, nayo haiwezi kutanguliwa isipokuwa mpaka wakati wa mwisho hapo
utakapokomeshwa wakati wote. 

Kama ilivyo MFANO [TYPE] wa raha ile inayosalia kwa
watu wa Mungu, yaani, raha ile ya milele, basi, haina budi kuendelea kwa nguvu zake zote
mpaka umilele ule utakapofika; kwa maana hakuna MFANO [TYPE] unaokoma mpaka hapo
KITU HALISI (ANTITYPE) kinapokuja. Zaidi ya hayo, sio dhahiri kwamba mtume huyu
anaitaja SABATO mahali hapa, iwapo ni ile ya Kiyahudi ama ile ya Kikristo; SABBATON
zake, ZA SABATO (ZA MAJUMA), inaelekea zaidi sana kuzihusu zile SIKUKUU ZA
MAJUMA walizokuwa nazo, ambazo mengi sana yamesemwa katika maelezo juu ya vitabu
vitano vya Musa (Pentateuch). ----- Toleo la l85l.
Dkt. Barnes, mfafanuzi wa Kanisa la Presbyterian ambaye alijulikana sana, anaandika hivi
katika maelezo yake ya 'NOTES ON COLOSSIANS (2:l6)':
"'[OR OF THE SABBATH DAYS] AU SABATO [yaani, SIKU ZA SABATO].' Neno hili
'sabato' katika Agano la Kale linatumika sio tu kwa siku ya saba, bali kwa siku zote za pumziko
takatifu ambazo zilishikwa na Waebrania, na hasa zile zilizotokea mwanzo na mwisho wa
sikukuu zao kuu. Pasipo shaka lo lote mahali hapa zinatajwa siku zile, kwa vile neno hili
[sabato] limetumika katika wingi, na mtume huyu haitaji hasa ILE Sabato inayoitwa hivyo
kihalali. Hakuna ushahidi wo wote kutokana na kifungu hiki kwamba angeweza kufundisha
kwamba hapakuwa na wajibu wo wote wa kushika wakati WO WOTE ulio mtakatifu, kwa
sababu hakuna sababu hata kidogo ya kuamini kwamba [Paulo] alimaanisha kufundisha
kwamba amri hii moja katika zile kumi ilikuwa imekoma kuwafunga wanadamu.

"Kama angelitumia neno hilo katika umoja 'THE SABBATH' [SABATO], hapo, kwa kweli,
ingekuwa wazi kwamba alikuwa na maana ya kufundisha kwamba amri ile ilikuwa imekoma
kuwa mojawapo ya masharti, na ya kwamba Sabato hiyo isingeweza kushikwa tena. Lakini
yale matumizi ya neno hilo katika wingi, na uhusiano wake, huonyesha ya kuwa jicho lake
[Paulo] lilikuwa linaziangalia zile siku nyingi zilizoshikwa na Waebrania kama sikukuu zao,
kama sehemu ya sheria yao ya Kafara na Kivuli (Ceremonial and typical law), na sio sheria ile
iliyohusika na maadili (Moral law), ama [yaani] zile Amri Kumi. Hakuna sehemu yo yote ya
sheria hii ya maadili ----- hakuna mojawapo ya amri hizo kumi ----- ambayo ingesemwa
kuwa ni 'KIVULI cha mambo [mema] yajayo.' Amri hizi, kulingana na tabia ya sheria hii ya
maadili, ni za milele na zinatoa wajibu kwa ulimwengu mzima." ----- Toleo la l850,
uk.306,307..

Kwa hiyo, baada ya kulichunguza Agano Jipya kwa makini, tunafikia mwisho wa kukata
maneno kwamba [fungu hilo] halina ushahidi wo wote kuhusu badiliko hilo la Sabato, hakuna
kibali cha Mungu kinachounga mkono badiliko kama hilo, wala hakuna kuungwa mkono ko
kote hata kama ni kwa kiwango kidogo kwa utunzaji huo wa siku ya Jumapili

 SWALI NINANI?LINI?SABATO YA JUMAMOSI ILIBADLISHWA KUWA JUMAPILI.
Yafuatayo nimaelezo juu ya kutoka sabato kwenda jumapili...............................................FUATILIA UJUE

Comments

Popular posts from this blog

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Chanzo cha saratani ya matiti