IJUE ASILI YA JUMAPILI NA IBADA YA JUA


TULIPO ISHIA KWA MAKALA ILIYO PITA
Sasa endelea.......
Badiliko toka Sabato ya kweli kwenda sabato ya uongo lililetwa na uasi mkuu uliotokea
katika kanisa la mwanzo ambalo liligeuka na kuwa katika mfumo wa Kikatoliki wa Rumi
[Roma]. Sababu zilizolisukuma kanisa hili kuitupilia mbali Sabato ya Bwana na kuichagua siku
ya waabudu jua zilikuwa mbili: nazo ni hizi, tamaa ya kuepuka kufananishwa na Wayahudi,
ambao ushupavu wao wa dini na anguko lao viliwafanya kuchukiwa na watu wote; na tamaa
yenye nguvu sawa na hiyo ni ile ya kutaka kuwaongoa wapagani waliokuwa wanaabudu jua na
kuwafanya washikamane na kanisa.

Hata katika siku zile za Mitume uasi huo ulianza kujitokeza. Paulo aliandika hivi: "Maana
ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi" (2 Wathesalonike 2:7).
Tena alitangaza hivi: "Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu
wakali wataingia kwenu wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu,
wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawandamie wao" (Matendo ya Mitume
20:29,30).

MPINGA KRISTO NDIYE MWASISI WA UTUNZAJI WA JUMAPILI
Ukengeufu huo kutoka katika imani ungeenea na kukua kwa kiwango kikubwa, alisema
Mtume huyo. "Ukengeufu" huo mkubwa, ama uasi, hatimaye ungemfunua "yule mtu wa kuasi
[mtu wa dhambi]," "mwana wa uharibifu; yule mpingamizi [Mpinga Kristo], ajiinuaye nafsi
yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu
la Mungu [Kanisa], akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu" (2
Wathesalonike 2:3,4).

Kwa kutimiza unabii huu uliotabiriwa, imani ya Kikristo na utawala wa kanisa la Kikristo
vikabadilika kabisa katikati ya siku zile za Mitume na kule kutangazwa kwa uongofu wake
Konstantino (Constantine), Mfalme wa Rumi [Roma]. Kweli ikabadilishwa na kuwa uongo, na
upotoshaji wa imani ile ya kweli uliongezeka kasi sana kwa kiwango cha kushangaza.
"Urembo wa ibada na kawaida za ibada ambazo wala Paulo, wala Petro hakupata kuzisikia,
zikaingia kanisani kimya kimya na kuanza kutumika, na baadaye zikadai kuwa zina cheo sawa
na zile zilizowekwa na Mungu. Maofisa [wa kanisa] ambao Mitume wale wa zamani
wasingeweza kupata mahali pa kuwaweka, pamoja na vyeo vyao ambavyo kwao [Mitume]
vingekuwa havina maana yo yote kabisa, vikaanza kuleta changamoto kwa watu, na kuitwa
kuwa ni vyeo vya Mitume." ----- WILLIAM D. KILLEN, D.D., THE ANCIENT CHURCH,
Utangulizi kwa Toleo la Kwanza, uk. xvi.
Miongoni mwa maadhimisho haya ya ajabu, mapya, na ya uongo yaliyoingizwa katika
kanisa lile lililoanguka, ilikuwa ni sikukuu ya Jumapili.
Kuhusu uasi huu, na mwanzo wa uadhimishaji huu wa siku ya Jumapili miongoni mwa
Wakristo ambao ulitokana na huo [uasi], pamoja na sababu zilizojificha nyuma ya kuichagua
sikukuu hii ya kipagani, ushuhuda mwingi sana wa kihistoria unaweza kuletwa. Kile
kilichotolewa hapa kimechukuliwa toka katika maandiko ya wale tu ambao wamekuwa au ni
WATUNZAJI WA SIKU HII YA JUMAPILI, kwa maana UNGAMO LAO kuhusu chanzo
cha utunzaji wake [Jumapili] litakuwa na uzito mkubwa zaidi kuliko shutuma ambazo
zingeweza kutolewa na wale WANAOITUNZA SABATO.

Wilhelm August John Neander, mwanathiolojia mkuu na mwanahistoria wa Kijerumani toka
Heidelberg, ambaye kitabu chake cha 'HISTORY OF THE CHRISTIAN RELIGION AND
CHURCH' kina thamani kubwa na sifa kiasi cha kumpatia cheo cha "mkuu wa wanahistoria
wa Kanisa," anatangaza kwa kusema kweli tupu:
"Upinzani kwa dini ile ya Kiyahudi ulisababisha kutangazwa kwa sikukuu maalum ya
Jumapili mapema sana, naam, ikiwa badala ya Sabato.... Sikukuu ya Jumapili, kama zilivyo
sikukuu nyingine zote, daima ilikuwa ni amri ya wanadamu tu, nayo ilikuwa mbali na makusudi
ya wale Mitume kuweza kuanzisha amri ya Mungu kwa njia kama hii, na tangu mwanzo wa
kanisa la Mitume wazo hili la kuhamisha sheria za Sabato kwenda Jumapili lilikuwa mbali nao.
Labda, mwishoni mwa karne ya pili ndipo matumizi potofu kama hayo yalianza kufanyika;
maana kufikia wakati ule watu wanaonekana kwamba walianza kufikiria kuwa kufanya kazi
siku ya Jumapili ilikuwa ni dhambi." ----- Rose's translation 
from the first German edition,
uk.l86.

AMRI  YA KWANZA YA JUMAPILI YA ZAMANI SANA IJULIKANAYO KATIKA HISTORIA.
Amri ya Jumapili ya zamani sana ijulikanayo katika historia ni ile ya Konstantino
iliyotangazwa mwaka 321 B.K. Inasomeka hivi:
"Katika siku tukufu ya jua hebu mahakimu na watu wale wanaokaa mijini wapumzike, na
viwanda vyote vifungwe. Walakini huko vijijini [mashambani] watu wale wanaoshughulika na
kilimo wanaweza kuendelea na kazi zao kwa uhuru na kwa kulindwa na sheria hii; kwa sababu
mara nyingi hutokea kwamba siku nyingine yo yote haifai sana kwa kupanda mbegu za nafaka
au kwa kupanda mizabibu; isije ikawa kwa kupuuzia wakati ule unaofaa kwa shughuli kama
hizo mibaraka ile ya mbinguni ikapotezwa. (Imetolewa siku ya 7 ya Machi, Krispo (Crispus) na
Konstantino (Constantine) wakiwa wote wawili wawakilishi wa Wananchi (Consuls) kwa mara
ya pili.) ----- CODEX JUSTINIANUS, lib.3, tit.l2,3; translated in PHILIP SCHAFF, D.D.,
HISTORY OF THE CHRISTIAN CHURCH (Seven-volume edition, l902), Vol.III, uk.380

Konstantino alikuwa Mfalme wa Rumi kuanzia mwaka 306 mpaka 337 B.K. Yeye alikuwa
mwabudu jua katika kipindi cha mwanzo cha utawala wake. Baadaye alijitangaza mwenyewe
kuwa ameongoka na kuwa Mkristo, lakini ndani ya moyo wake aliendelea kuwa mshabiki wa
kuabudu jua.
Kuhusu dini yake, Edward Gibbon, katika kitabu chake cha 'THE DECLINE AND FALL
OF THE ROMAN EMPIRE, asema hivi:
"Ushabiki wa dini wa Konstantino ulielekezwa kwa bidii zaidi kwenye jua, Apolo (Apollo)
wa miungu ya Wayunani na Warumi; naye [Konstantino] alipendezwa kuwakilishwa kwa
ishara za mungu huyo wa nuru na mashairi. Mishale isiyokosea ya mungu huyo, mng'ao wa
macho yake, taji yake ya heshima, uzuri wake usiokoma, na mafanikio yake mazuri,
vilionekana kumsonda kidole [huyo Apolo] kama ndiye mlezi (patron) wa Shujaa huyo kijana.
Madhabahu za Apolo zilistawishwa kwa sadaka zilizotolewa na Konstantino kama nadhiri yake;
na umati wa watu wale wajinga walifundishwa kusadiki kwamba Mfalme yule aliruhusiwa
kuangalia kwa macho yake ya kibinadamu utukufu wa mungu wao mlinzi; na kwamba, aidha
anapoamka au anapokuwa katika maono alikuwa anabarikiwa na heri za ndege njema [bahati]
ya utawala wake mrefu na wenye ushindi. Jua lilisherehekewa ulimwenguni kote kama ndiye
kiongozi asiyeshindikana na mlinzi wa Konstantino." ----- Sura ya 20, aya ya 3
Kufuatia amri hiyo ya awali, wafalme wote na mapapa wote katika karne zile zilizofuata
waliongeza amri nyingine za kuimarisha utunzaji wa Jumapili.
"Walakini, kile kilichoanza kama amri ya kipagani, kikaisha kama amri ya Kikristo;

msururu mrefu wa amri za kifalme katika karne ile ya nne, ya tano, na ya sita, zikaamuru kwa
ukali kujizuia kufanya kazi siku ya Jumapili." ----- Kitabu kile kile (ibid.) uk.270.

Hatua hizi za ziada ambazo kanisa na serikali walizichukua kuhakikisha ya kwamba
Jumapili inakuwa badala ya Sabato kwa lazima, zimeelezwa katika aya chache tu na
mwanasheria maarufu wa Baltimore, Maryland, aitwaye James T. Ringgold:

"Katika mwaka 386, chini ya Gratian, Valentinian, na Theodosio (Theodosius), iliamriwa
kwamba mashauri [daawa] yote mbele ya sheria pamoja na shughuli zote hazina budi kukoma
[siku ya Jumapili]....

"Miongoni mwa mafundisho ya dini yaliyoandikwa katika waraka wa Papa Innocent I,
ulioandikwa katika mwaka wake wa mwisho wa upapa (4l6), ni kwamba siku ya Jumamosi
[Sabato] iadhimishwe kama siku ya kufunga [kuacha kula chakula] tu....

"Katika mwaka 425, chini ya Theodosio Kijana, kujizuia kufanya michezo ya kuigiza
(theatricals) pamoja na kutofanya tamasha (circus) [Jumapili] kuliamriwa....
"Mwaka 538, katika Baraza la Orleans,... iliagizwa kwamba kila kitu kilichoruhusiwa siku
za nyuma kufanyika siku ya Jumapili kiendelee kuwa halali; bali kwamba kazi ya kulima kwa
plau, au katika mashamba ya mizabibu, kukata majani, kuvuna, kupura nafaka, kulima, na
kuweka boma la miti viepukwe kabisa, ili watu waweze kuhudhuria kanisani kwa raha zaidi....
"Karibu na mwaka 590 Papa Gregory, katika waraka wake kwa Warumi, aliwashutumu
kuwa ni manabii wa Mpinga Kristo wale waliosisitiza kuwa kazi isingepaswa kufanywa siku ile
ya saba." ----- THE LAW OF SUNDAY, Uk..265-267.
Aya ya mwisho ya kufungia maneno yaliyonukuliwa juu huonyesha kwamba bado
walikuwamo ndani ya kanisa hadi kufikia mwaka 590 B.K. wale ambao walikuwa wanaitunza
na kuwafundisha wengine kuitunza Sabato ya Biblia. Kusema kweli, utunzaji kama huo kwa
wale wachache umefuatwa katika karne zote za Kikristo. Miongoni mwa wale walioitwa
Waldensia (Waldenses) walikuwamo watunzaji wa siku ya saba.

Neander anauliza swali hili:
"Je, tusiweze kudhani kwamba tangu zamani za kale kikundi cha Wakristo wanaofuata
desturi za Kiyahudi kilisalia, ambacho kutokana nacho madhehebu hii [ya Wapasaginia
(Pasaginians), waliowekwa katika kundi moja na Waldensia na baadhi ya waandishi
wanaoaminika] inapaswa kufikiriwa kama tawi lao?" ----- CHURCH HISTORY, FIFTH
PERIOD, Section 4, l5th American ed., Vol. IV, uk. 59l.
Amri za kidini na serikali zilizotajwa sasa hivi katika kuianzisha amri ya Jumapili
zinaliweka suala hili kwa wazi sana hata Eusebio, Askofu maarufu wa Kanisa Katoliki, baba
mmoja mwenye kusifika wa historia ya kanisa, na mwenye mazoea ya kujipendekeza mno kwa
Konstantino na mwandishi wa habari za maisha yake, alikuwa na haki kusema hivi:

"Mambo yo yote ambayo yalikuwa ni wajibu kufanyika siku ya Sabato, hayo sisi
tumeyahamishia katika Siku ya Bwana [Jumapili]." ----- COMMENTARY ON THE
PSALMS, COMMENT ON PSALMS 9l (92 IN AUTHORIZED VERSION), quoted in
ROBERT COX, LITERATURE OF THE SABBATH QUESTION, Vol.I, uk. 36l.
KUIWEKA SIKU YA KIPAGANI MAHALI PA SIKU YA MUNGU

Huku kuiweka Jumapili badala ya Sabato sio jambo ambalo Kanisa Katoliki linakana au
linajaribu kuficha. Kinyume chake, linakiri wazi, na kwa kweli linaonyesha kitendo hicho kwa
majivuno kuwa ni ushahidi wa uwezo wake wa kubadili hata amri ya Mungu. Soma maneno
haya yaliyonukuliwa kutoka katika Katekesimo za Kikatoliki:
THE CONVERT'S CATECHISM OF CATHOLIC DOTRINE, kazi ya Reverend Peter
Geiermann, C.S.R., Januari 25, l9l0 ilipokea "mbaraka wa kitume" wa Papa Pius wa X. Juu ya
somo hili la badiliko la Sabato, Katekesimo hii inasema hivi:
"SWALI. ----- Siku ya Sabato ni siku gani?
"JIBU. - ---- Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
"SWALI. ----- Kwa nini tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi?
"JIBU. ----- Tunaitunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki, katika
Baraza la Laodikia (336 B.K.), lilihamisha taratibu ya ibada kutoka Jumamosi kwenda
Jumapili." ----- Toleo la pili, uk. 50.
A DOCTRINAL CATECHISM, iliyoandikwa na Reverend Stephen Keenan, iliidhinishwa
na Most Reverend John Hughes, D.D., Askofu Mkuu wa New York. Inayo maneno haya
kuhusu suala hili la badiliko la Sabato:

"SWALI. ----- Unayo njia nyingine yo yote ya kuthibitisha kwamba kanisa linao uwezo wa
kuanzisha sikukuu ambazo zinashikwa kama amri?
"JIBU. ----- Kama lisingekuwa na nguvu kama hizo, lisingaliweza kufanya kile ambacho
wanadini wote wa siku hizi wanakubaliana nacho ----- lisingaliweza kuweka utunzaji wa
Jumapili siku ya kwanza ya juma mahali pa utunzaji wa Jumamosi siku ya saba, badiliko
ambalo halina Maandiko yo yote yanayolipa kibali hicho." ----- Ukurasa l74.

AN ABRIDGMENT OF THE CHRISTIAN DOCTRINE, iliyoandikwa na Reverend Henry
Tuberville, D.D., wa Chuo cha Douay, Ufaransa, ina maswali na majibu haya:
"SWALI. ----- Unathibitishaje wewe kwamba kanisa linao uwezo wa kuamuru sikukuu na
siku takatifu?
"JIBU. ----- Kwa kitendo kile kile cha kuibadili Sabato kuwa Jumapili, kitendo ambacho
Waprotestanti wanakikubali; na kwa hiyo wanajikanusha wenyewe kijinga, kwa kuitunza
Jumapili kwa ukali, na kuzivunja karibu sikukuu nyingine nyingi sana zilizoamriwa na Kanisa
lilo hilo.
"SWALI. ----- Unalithibitishaje hilo?
"JIBU. ----- Kwa sababu kwa kuitunza Jumapili, wanaukiri uwezo wa Kanisa wa kuamuru
sikukuu, na kuziamuru chini ya sharti la dhambi; na kwa kule kutozitunza zile zilizobaki
[katika sikukuu] ambazo zimeamriwa nalo, kwa kweli, wanaukana tena uwezo ule ule." -----
Ukurasa 58.

HAKUNA FUNGU HATA MOJA LA BIBLIA KWA KUITUNZA JUMAPILI
Kadinali Gibbons, katika kitabu chake cha 'THE FAITH OF OUR FATHERS,' asema hivi:

"Unaweza kusoma Biblia toka Mwanzo hadi Ufunuo, nawe hutalipata fungu [mstari] hata
moja linaloidhinisha utakatifu wa Jumapili. Maandiko yanaamuru utunzaji wa kidini wa siku
ya Jumamosi, siku ambayo sisi hatuitakasi kamwe." ----- Toleo la l893, uk.11

"KANISA KATOLIKI... LILIBADILI SIKU"
Gazeti la 'CATHOLIC PRESS' la Sydney, Australia linasisitiza kwamba utunzaji wa
Jumapili asili yake ni ya Kikatoliki peke yake.
"Jumapili imewekwa na Wakatoliki, na madai yake ya kuitunza yanaweza kutetewa tu kwa
kanuni za Kikatoliki.... Toka mwanzo mpaka mwisho wa Maandiko [Biblia] hakuna hata
kifungu kimoja cha maneno ambacho kinaunga mkono uhamishaji huo wa ibada ya [watu]
wote ya kila juma toka siku ya mwisho wa juma kwenda siku ya kwanza." ----- Agosti 25,
l900.
Katika kitabu chake cha 'PLAIN TALK ABOUT PROTESTANTISM OF TODAY,'
Monsignor Segur asema hivi:
"Lilikuwa ni Kanisa Katoliki ambalo, kwa idhini ya Yesu Kristo, lilihamisha pumziko hili
kwenda Jumapili kwa ukumbusho wa ufufuo wa Bwana wetu. Hivyo utunzaji wa Jumapili kwa
Waprotestanti ni kuisujudia (pay homage) mamlaka ya Kanisa [Katoliki], kinyume chao
wenyewe." ----- Toleo la l868, Sehemu ya 3, Kifungu cha l4, uk.225.
Katika mwaka l893 gazeti la 'CATHOLIC MIRROR' la Baltimore, Maryland lilikuwa
chombo rasmi cha Kadinali Gibbons. Katika toleo lake la Septemba 23 la mwaka ule
lilichapisha usemi huu wa kushangaza sana:

"Kanisa Katoliki kwa zaidi ya miaka elfu moja kabla ya kuwako Mprotestanti hata mmoja,
kwa utume wake mtakatifu, lilibadili siku toka Jumamosi kwenda Jumapili." "Kwa hiyo,
Sabato ya Kikristo [Jumapili] mpaka leo hii inakubalika kama mtoto wa Kanisa Katoliki likiwa
mke wa Roho Mtakatifu, wala hakuna neno hata moja la kugombeza kutoka kwenye ulimwengu
huo wa Kiprotestanti." ----- Reprinted by the CATHOLIC MIRROR as a pamphlet, THE
CHRISTIAN SABBATH, uk. 29,3l.

UTUNZAJI WAJUMAPILI HAUNA KIBALI MBELE ZA MUNGU

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Chanzo cha saratani ya matiti