Mugabe kuelekea Afrika Kusini kutatua kesi ya mke wake

Rais Mugabe na mke wake Grace

Mtandao wa habari nchini Afrika Kusini wa Eyewitness News, unasema kuwa Rais Robert Mugabe amebadilisha mipango yake ya safari kuweza kushughulikia suala linalomhusu mkewe nchini Afrika Kusini.
Msichana wa umri wa miaka 20 amemlaumu mke wake Mugabe, Grace kwa kumpiga kwa kifaa cha umeme wakati wa mzozo kwenye hoteli moja Jumapili jioni.
Bi Mugabe hakufika katika kituo cha polisi mjini Johannesburg baada ya kusema kuwa angefanya hivyo na hadi sasa hajazungumza lolote kuhusu madai hayo.
Kinyume na ripoti za awali kuwa Bi Mugabe alikuwa amerejea nchini Zimbabwe, mtandao wa Eyewitness pia unasema kuwa Bi Mugabe yuko bado nchini Afrika Kusini.
Rais Mugabe anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) mjini Pretoria wiki hii.chanzo cha habari

Comments

Popular posts from this blog

Kanuni za kuishi na Watu / Binadam Vizuri

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.

Chanzo cha saratani ya matiti