Nampenda sana Vanessa: Jux

Alipoulizwa na mtandao huu kuhusu uhusiano wake na Vanessa, alisema: ”Nampenda Vanessa kuliko msichana yeyote yule na sitegemei kumuacha, hata familia yangu inajua kuwa nina upendo Mkubwa kwa Vanessa.
“Nikiwaga mbali na Vanessa huwaga asubuhi nikiamka cha kwanza naingiaga Instagram kumuangalia baada ya hapo ndo nampigia simu siwezi, kumpigia simu bila kuangalia picha zake. Kiufupi nampenda sana Vanessa,“ alisema Jux.
Kuhusu kupata mtoto, Jux alifunguka kwamba: “Sa’hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo kwa sasa wa kujipanga kupata mtoto na mpenzi wangu pia mtoto wangu wa kwanza nataka nimuite jina la Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.”
Comments
Post a Comment