Njia za Kujikinga na Magonjwa ya Moyo
Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases) yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika nchi za Afrika kinyume miaka ya nyuma. Kati ya sababu mojawapo ni mabadiliko katika mitindo ya maisha na lishe. Watu wengi hawana mazoezi na wanakula vyakula vyenye nishati nyingi (energy dense diet) kuliko vyenye virutubisho kwa wingi (nutrient dense diet), na hili linachangia sana kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa haya. Labda unajiuliza ni magonjwa gani haya? Hapa tunaongelea magonjwa kama shinikizo la damu la kupanda (presha au hypertension), kiharusi (stroke), moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure), moyo kuwa mkubwa, shambulio la moyo (heart attack) na mengineyo. Zikiwemo sababu nyingine, magonjwa haya kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mitindo ya maisha na lishe. Njia Za Kuzuia Magonjwa Ya Moyo Na Mishipa Ya damu Kwa kubadili mtindo wako wa maisha unaweza kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, au usiyapate kabisa. Zingatia mambo yafuatayo kujikinga na magonjwa ...
Comments
Post a Comment