Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases) yamekuwa yakiongezeka kwa kasi katika nchi za Afrika kinyume miaka ya nyuma. Kati ya sababu mojawapo ni mabadiliko katika mitindo ya maisha na lishe. Watu wengi hawana mazoezi na wanakula vyakula vyenye nishati nyingi (energy dense diet) kuliko vyenye virutubisho kwa wingi (nutrient dense diet), na hili linachangia sana kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa haya. Labda unajiuliza ni magonjwa gani haya? Hapa tunaongelea magonjwa kama shinikizo la damu la kupanda (presha au hypertension), kiharusi (stroke), moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure), moyo kuwa mkubwa, shambulio la moyo (heart attack) na mengineyo. Zikiwemo sababu nyingine, magonjwa haya kwa kiasi kikubwa huchangiwa na mitindo ya maisha na lishe. Njia Za Kuzuia Magonjwa Ya Moyo Na Mishipa Ya damu Kwa kubadili mtindo wako wa maisha unaweza kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, au usiyapate kabisa. Zingatia mambo yafuatayo kujikinga na magonjwa ...
Haki miliki ya picha ALAMY Image caption Baadhi huamini michoro iliyo kwenye dola za Marekani ina uhusiano na Illuminati Ni simulizi ya ulaji njama ambayo bila shaka imevuma zaidi kushinda njama nyingine zote. Ni wachache sana ambao hawajawahi kusikia kuwahusu Illuminati. Huaminika kuwa kundi maalum la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia, na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia. Kwa wengine, wamehusishwa na utajiri wa ghafla ambao si wa kawaida. Ukitajirika haraka, kunao bila shaka watakaodai kwamba umejiunga na Illuminati. Je, kuna ukweli wowote kuhusu wasiwasi huu? Kuna kundi la watu wanaofanya vikao vya siri kupanga njama za kuitawala dunia na pia kjifaidi wenyewe kwa pesa na utajiri? Simulizi hizi na umaarufu wa illuminati zina ukweli wowote? Wasiwasi huu kuhusu kundi linalopanga njama ya kuweka utawala mpya duniani ulianza miaka ya 1960, sana kutokana na ubunifu wa watu fulani. Kuenea kwa habar...
Haki miliki ya picha ESO Image caption Mchoro wa Oumuamua Wataalamu wanaofanya kazi katika mradi unaotafuta iwapo kuna dalili za kuwepo kwa viumbe anga za juu wanajiandaa kuchunguza sayari ndogo inayopita katika mfumo wetu wa jua kubaini iwapo kuna uwezekano wa viumbe kama hao kuwepo. Sayari hiyo ndogo yenye umbo ambalo si kawaida kwa sayari iligunduliwa ikielekea kwenye mfumo wa jua siku ya Jumapili 19 Oktoba. Ndiyo sayari ya kwanza kutoka kwa mfumo mmoja wa nyota iliyoingia kwenye mfumo mwingine wa nyota ambayo imetambuliwa kufikia sasa. Sifa zake zinaonesha kwamba imetoka kwenye mfumo wa nyota nyingine. Mpango huo ambao unaungwa mkono na bilionea Yuri Milner utatumia tadubini inayotumia miali ya redio kujaribu kupata mawasiliano kutoka kwa sayari ndogo hiyo Juhudi za kundi hilo la wataalamu zitaanza leo Jumatano, ambapo wataalamu wa anga za juu wataitazama sayari ndogo hiyo, ambayo kwa sasa inasonga kwa kasi kuupita mfumo wetu wa jua. Sayari ndogo hiyo itafuatiliwa kw...
Comments
Post a Comment