Posts

Showing posts from March, 2018

KUWA MBUNIFU UFANIKIWE MAISHANI MWAKO

Image
Katika maisha yako yote ambayo uaytaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu basi  utaendelea kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati  katika maisdha yako ni lazima uwe mbunifu. Ubunifu ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo tayakuwa ni ya kawaida tu. Kwa sababu  katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu ambacho  unakifanya wewe kwa asilimia kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa mfanano wa vitu unazidi kuongeze swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni, hivi natajitautishaje na wenzangu? Majibu ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha kivingine unachotakiwa kufanya ni kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja kifua

KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA HUDHOOFISHA MWILI

Image
Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu. Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari, hapa nimeweka chumvi kidogo lakini huo ndio ukweli halisi. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono. Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana. Twende pamoja katika k

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe Kwako

Image
Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule. 1. Uwezo wako wa nishati Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufik

JE! CHAKULA KINAWEZA KUATHIRI AKILI YAKO? (SOMA DANIELI 1 YOTE)

Amini usiamini, chakula kinaweza kuathiri akili yako, na afya yako ya kimwili na kiroho. Kwa maelezo zaidi juu ya somo hili la afya soma vitabu vya Afya na Lishe, kama vile Afya na Raha na Uponyaji wa Mungu ambamo zimefafanuliwa Kanuni 8 za Afya ----- Lishe bora, Mazoezi ya mwili, Hewa safi, Maji safi na salama, Mwanga wa jua, Pumziko, Kiasi, na Kumwamini Mungu. Ukizifuata utaepukana na magonjwa mengi na kupunguza gharama ya matibabu. Yatabaki magonjwa yanayokuja kwa njia zingine zisizozuilika. Chakula cha daraja la kwanza ambacho Mungu alimpa mwanadamu kilikuwa cha nafaka, kokwa na matunda (Mwanzo 1:29). Dhambi ilipoingia ilileta laana sio tu kwa viumbe vyote bali hata kwa ardhi. Kwa hiyo Mungu akamwongezea mwanadamu mboga za majani katika lishe yake ya awali (Mwanzo 3:18). Gharika ilikaa juu ya nchi kwa miezi mitano au siku 150 na kuharibu mimea yote (Mwanzo 7:24). Kwa hiyo Mungu akamwongezea mwanadamu katika lishe yake "nyama" kutoka kwa

MFALME WA AMANI ANAKUJA UPESI SANA (SOMA DANIELI 2 YOTE)

Hakuna mwanadamu ye yote awezaye kutabiri kwa hakika mambo yatakayokuja baadaye kwa hekima au maarifa yake mwenyewe. Wanajimu [wanaobashiri kwa kuangalia nyota], wachawi wanaotazama bao, wasoma viganja, hata wana sayansi wanabahatisha tu, hawawezi kujua kwa hakika mambo ya zamani au mambo yanayokuja mbele (Dan.2:27,28; Isa. 42:8,9; 46:9,10; 41:21-24; 8:19; Yak. 4:13-16).  Ni Mungu peke yake anayejua mambo ya zamani na yale yajayo, naye anatuambia kabla hayajatokea. Tangu dhambi iingie duniani mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu yalikatika; anawasiliana nasi kupitia kwa manabii anaowachagua mwenyewe (Isa.59:2; Hes. 12:6). Matukio yote makubwa yanayoleta maafa kwa wanadamu anawajulisha manabii wake (Amosi 3:7). Kuhusu Gharika alimjulisha Nuhu; kuangamizwa kwa Ninawi alimjulisha Yona; kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora alimjulisha Ibrahimu. Mbele yetu kuna mapigo saba (Ufunuo 16) ambayo yatawaathiri sana wanadamu. Kabla hayajaja alimjulisha Yohana kisiwa