Posts

Showing posts from May, 2020

Idadi ya wagonjwa wa corona nchini Kenya yafikia 1,214 baada ya kutangazwa wagonjwa wapya 22

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Wagonjwa wapya 22 wa corona wamethibitishwa Kenya Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona Kenya imefikia 1,214, baada ya wagonjwa wapya 22 kuthibitishwa siku ya Jumapili. Wakati wa mkutano na vyombo vya habari , katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman amesema kwamba wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 24 hadi 73 ,huku, wanaume wakiwa 17 na wanawake wakiwa watano. Akitoa habari njema , Dkt Aman amesema kwamba wagonjwa watatu waliondoka hospitalini na hivyo basi kufanya idadi ya wagonjwa waliopona virusi hivyo kufikia 383. Amesema kwamba mgonjwa mmoja ambaye aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika eneo la Mathare alifariki, na kufanya idadi ya waliokufa nchini humo kufikia watu 51. Amesema kwamba idadi ya watu waliopimwa virusi hivyo kufikia sasa ni 59,260. Amesema kwamba wagonjwa 10 wanatoka katika mji wa Nairobi, 9 wanatoka Mombasa, mmoja anatoka Kwale na Nakuru na Taita taveta yakiwa na mgonjwa mmoja mmoja

Virusi vya corona: Mashine ya kupima corona 'yakutwa na hitilafu Tanzania'

Image
Haki miliki ya picha @UMWALIMU Wizara ya afya nchini Tanzania imetangaza kwamba uchunguzi wa serikali uliokuwa ukifanywa katika maabara kuu ya nchi hiyo umebaini kuwa moja ya mashime ya kupima corona ilikuwa na hitilafu. Waziri Ummy Mwalimu hii leo ametangaza matokeo ya uchunguzi aliyoagiza kufanyika baada ya Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kutilia shaka ufanisi wa maabara hiyo. "Kamati imebaini kuwepo kwa mapungufu ya uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo na uhakiki wa ubora wa majibu'' amesema Waziri Mwalimu. Pia kumebainika kuwepo kwa udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya covid-19, aidha imebainika kuwepo kwa upungufu wa Wataalamu"- Waziri Afya Ummy mwalimu amesema. Wizara ya afya nchini humo imeweka wazi kwamba sasa vipimo vitakuwa vinafanyika katika maabara iliyopo mabibo. "Kuanzia sasa shughuli zote za upimaji wa maabara ya taifa zitafanyika katika maabara mpya ya mabibo yenye vifaa vya kisasa vyenye ubora na uwezo wa kupima sam

KINA MAMA ACHENI KUTOA MIMBA KWA MAKUSUDI SOMA KISA CHA MAMA HUYU Martha Anne-Bowre mwanamke anayejuta kuavya mimba 5 kwa makusudi

Image
Haki miliki ya picha MAMA MARTHA ANNE-BOWRE Uavyaji (utoaji) mimba ni kinyume cha sheria katika baadhi ya mataifa barani Afrika jambo ambalo limekuwa likichangia wasichana na hata wanawake kutafuta njia za siri na ambazo ni hatari kulitekeleza hilo. Martha Anne Bwore mwanaharakati anayepinga uavyaji mimba nchini Kenya aliye na miaka 55 anaeleza namna hofu na mahangaiko wanayopitia wasichana wakati wanapoachwa bila mawaidha au muongozi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na tendo la ndoa vinavyopelekea uavyaji mimba. Na ni jambo ambalo analifahamu kwa uzito wake, kutokana na kuipitia hali kama hiyo na kuishia kuavya sio mimba moja wala mbili, lakini sita. Japo kati ya hizo mimba moja ilibidi atolewe ili kuokoa maisha yake. Kilichomshinikiza, anaeleza ni matamanio ya kupata mpenzi wa kuishi naye, kwani wapenzi aliobahatika kuwa nao walimshinikiza kuavya mimba ili kuendeleza mahusiano hayo. Uhuru wa maisha kwa mara ya kwanza Haki miliki ya picha GIANLUIGI GUERCIA Bi Martha anas

Virusi vya Corona: China yaionya Marekani dhidi ya kusababisha vita baridi

Image
Haki miliki ya picha China yaionya Marekani dhidi ya kusababisha vita baridi Waziri wa masuala ya kigeni nchini China ameishutumu Marekani kwa kueneza dhana potofu na uongo kuhusu virusi vya corona hatua inayozua hofu kati ya mataifa hayo mawili. Marekani imeambukizwa na 'virusi vya kisiasa' vinavyowasukuma baadhi ya wanasiasa kuishambulia mara kwa mara China ,Wang Yi aliambia maripota siku ya Jumapili. Aliitaka Marekani kuacha kupoteza wakati pamoja na maisha ya watu wasio na hatia katika vita vyake dhidi ya Covid-19. Hali ya wasiwasi kati ya Washington na Beijing imeongezeka huku virusi hivyo vikisambaa. Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu amekosolewa kwa jinsi anavyopigana vita vyake dhidi ya ugonjwa huo na amelaumu China kwa kujaribu kuficha mlipuko huo. Lakini siku ya Jumapili, Bwana Wang alirejelea msimamo wa China kwamba taifa hilo lilichukua hatua zilizohitajika kukabiliana na virusi hivyo tangu viliporipotiwa mwezi