Posts

Showing posts from September, 2017

Je wanawake wanaweza kuibadili dunia kwa wiki?

Image
Haki miliki ya picha Msimu mpya wa wanawake 100 wa BBC umerudi kwa kishindo. Mpaka sasa majina 60 ya kwanza yametangazwa, akiwemo mwana anga za juu wa Nasa Peggy Whitson, Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia. msanii Tiwa Savage wa NIgeria na mchezaji soka wa England Steph Houghton. Majina mengine 40 yataongezwa katika msimu huu mwezi Oktoba. Makala haya ya kila mwaka - yanayoangazia masuala yanayowahusu wanawake kote duniani inahimiza wanawake mwaka huu kufanya mabadiliko. Orodha hiyo inajumuisha pia mshairi Rupi Kaur, muathiriwa wa shambulio la tindi kali Resham Khan na mtumbuizaji Jin Xing. Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Jin Xing Visa vinavyoonekana kutomalizika vya unyanyasaji, ukosefu wa usawa, na kutoonekana kwa wanawake katika nyanja nyingi za kijamii, kunasababisha hisia ya kutowezeshwa wanawake na inavunja moyo. Kwahiyo mwaka huu tunawataka wanawake kutoa njia za kukabiliana na mambo hayo yanayochangia ukosefu wa usawa kwa wanawake. Ikiwa ni mwa

Rapa B.o.B ataka kuthibitisha iwapo dunia ni duara

Image
Haki miliki ya picha NASA Mwanamuziki wa Marekani wa mtindo wa rap B.o.B. anatafuta msaada wa kutuma satelaiti kuthibitisha iwapo kweli dunia ni duara. Rapa huyo ambaye jina lake halisi ni Bobby Ray Simmons Jr, ni mmojawapo ya watu wanaoamini kwamba dunia ni kama sahani na sio duara. Baadhi ya wanaomini kuwa dunia ina umbo la sahani wanaodaia wafanyakazi wa NASA shirika la wana anga za juu wanalinda ukingo wa dunia kuzuia watu wasianguke. Anajaribu kuchangisha $200,000 katika mtandao wa kuchangisha fedha wa GoFundMe na mpaka sasa amefanikiwa kukusanya kima cha $650, lakin kampeni hiyo imekuwa ikizungumziwa kwamapana katika mtadao huo. Image caption Msanii wa Marekani B.o.B 'Nionyeshe upinde' "Nimeanzisha kampeni hii kwasababu ningependa kutuma kama sio satelaiti moja basi nyingi katika anga za juu kujaribu kutafuta upinde unaoifanya dunia kuwa duara," alisema katika video iliowekwa kwenye mtandao huo. "Nautafuta upinde," ameongeza B.o.B

Teksi ndege isiokuwa na rubani yazinduliwa Dubai

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed. Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isio na rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini. Ndege hiyo isio na rubani yenye nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya ghuba. Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed. Dubai ina malengo makubwa ya kuwa mji wa kiteknolojia huku ndege zisizo na rubani na roboti zikihusika pakubwa katika mpango huo Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano. ''Utumizi wake utahusisha simu aina ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo unalopania kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter. Image caption Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio

Mwanzilishi wa jarida la Playboy aaga dunia

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Hugh Hefner alifariki kwa amani nyumbani kwake Hugh Hefner, mwanzilishi wa jarida la kimataifa la watu wazima - Playboy, amefariki akiwa na umri wa miaka 91. Playboy Enterprises Inc imesema alifariki kwa amani nyumbani . Hefner alianza kuchapisha jarida hilo jikoni nyumbani mwake mnamo 1953. Likawa jarida linalo uzika zaidi la wanaume duniani. Cooper Hefner, mwanawe amesema "atakumbukwa kwa ukubwa na wengi". Alimtaja babake kama "Mojawapo ya watu wa kwanza kujitosa katika uandishi na aliishi maisha ya aina yake na yenye utofuati," na amemuita mtu anayetetea uhuru wa kuzungumza, haki za kiraia na uhuru wa kijinsia. Mnamo 2012, akiwa na umri wa 86, alimuoa mke wake wa tatu Crystal Harris - ambaye alikuwa mdogo wake kwa miaka 60. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mkewe wa wa tatu Crystal Harris anamrithi Jarida la Hefner lilichangia kile kinachoonekana kuwa kuheshimiwa kwa picha za utupu katika vyombo v

Wabunge watwangana makonde Uganda

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika siku ya pili ya kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo. Katika ugomvi huo wabunge hao walirushiana viti, kuharibu vipaza sauti na katika kikao hicho kilichoongozwa na Spika wa bunge, Bi.Rebecca Kadaga. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Wabunge watwangana makonde ukumbini Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Wabunge wapambana Ugomvi huo ulianza pale Spika alipochukua hatua ya kuwafukuza wabunge wapatao 25 wengi wao wakiwa ni wale wa upinzani kwa madai ya utovu wa nidhamu pamoja na waziri wa serikali aliyeshtakiwa kwa kufyatua risasi bungeni siku ya jumanne. Wabunge hawa wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa basi rais aliyepo kwa sasa atapata mwanya wa kugombea tena mwaka 2021

Mwanamke ajioa nchini Italia

Image
Haki miliki ya picha  MARTINI Image caption Furaha yangu haitegemei uwepo wa mwanamume Mwanamke moja nchini Italia amejioa yeye mwenyewe kwenye sherehe iliyokuwa na vazi kamili la harusi, keki na wageni 70. "Ninaamini kuwa kila mmoja wetu ni lazima ajipende," alisema Luara Mesi mwenye miaka 40 Wanaounga mkono ndoa kama hizo wanasema kuwa suala kuu ni kujipenda. Mwanamke ajioa baada ya kukosa mchumba Laura anasema kuwa suala la kujioa lilimkujia miaka miwili iliyopita, baada ya miak 12 ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. Haki miliki ya picha MICAELA MARTINI Image caption Ndoa ya Bi Mesi "Niliwaambia marafiki zangu na familia kuwa sijapata mpenzi na nikiwa na umri wa miaka 40 nitajioa." aliliambia gazeti la La Repubblica. "Ikiwa siku moja nitapata mwanamume ambaye nitapanga kuishi naye nitafurahi, lakini furaha yangu haimtegemei yeye." Bi Mesi anasema kuwa yeye ndiye mwanamke wa Kwanza nchini Italia kufanya harusi ya mtu mmoja. Haki

Kabla ya kufunga ndoa hakikisha mmepima haya magonjwa 4 ya kuambukizwa

Image
1. Ugonjwa wa kaswende. Kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri. Kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa. 2. Ugonjwa wa hepatitis B. Ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi. Ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani

Alichokisema Polepole kuhusu Madiwani wa Chadema waliohamia CCM

Image
Dar es Salaam. Siku chache baada ya diwani mwingine wa Chadema mkoani Arusha kujiunga na CCM, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amesema tukio hilo halikuwa limeandaliwa. Diwani huyo wa Kimandolu (Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi alitangaza kuihama Chadema dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa fursa kwa wanachama wa vyama tofauti kutangaza kujiunga na vyama vingine. Tukio hilo lilifanyika wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maofisa 422 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Baada ya tukio hilo la madiwani, wabunge wa Chadema, Godbless Lema(Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) walijitokeza kukemea kitendo cha kutumia shughuli ya kiserikali kujenga chama na kwamba wana taarifa kuwa rushwa ilitumika na wanao ushahidi wa kumuonyesha Rais. Pamoja na Rais kueleza katika hotuba yake kuwa ameambiwa kuwa kulikuwa na watu wanataka kujiunga na CCM, Polepole amba

Kwanini hauna pesa? Soma hapa

Image
Inawezekana ukawa unafanya kazi ama biashara nzuri inayokuingizia kipato cha kutosha lakini kutokana na sababu usizozijua huwa ukijikuta ni mtu wa kuishiwa na kujikuta kuwa huna pesa. Kama umekuwa ukiishi hivi na kuwa mtu wa kuishiwa na kushindwa kuwa na pesa za kutosha, makala hii ni muhimu sana kwako. Je, unajua ni sababu zipi zinakufanya ushindwe kuwa na pesa ya kutosha katika maisha yako? Hizi hapa Una tabia mbaya zinazokuzuia kupata pesa. Kama ulevi, Matumizi mabaya ya pesa, kuangalia TV kwa muda mrefu. n.k Unazungukwa na watu wengi ambao sio sahihi kwako. Umekuwa mwongeaji sana bila kuchukua hatua. Hauna mipango maalumu. Umekuwa ukikata tamaa mapema. Umekuwa ni mtu wa kupoteza muda sana. Umekuwa huna tabia ya kujiwekea akiba.

Jinsi Ya Kujua Fursa Za Kibiashara Zinazokuzunguka Hapo Ulipo Sasa

Image
Watu wengi wanapopanga kuanzisha biashara, huwa wamekuwa wakihangaika na kutafuta wazo lipi bora la biashara kwao kufanya. Wengi hutafuta fursa kubwa na za mbali na kusahau fursa za karibu ambazo zinawazunguka kila siku kwenye maisha yako. Kwenye makala ya leo ya ushauri wa changamoto, tutakwenda kujadili jinsi unavyoweza kujua fursa za kibiashara ambazo zinakuzunguka hapo ulipo sasa. Iwe ni kazini, mtaani au hata kwenye biashara ambayo tayari unaifanya. Zipo fursa nyingi zinazokuzunguka hapo ulipo sasa. Kabla ya kuangalia namna unavyoweza kuzitumia fursa zinazokuzunguka, tupate maoni kutoka kwa msomaji mwenzetu; Changamoto yangu ni mbinu za kufanya biashara na kupata faida. Namna ya kupata fursa katika eneo lolote la biashara. Jerome J. K. Kama alivyouliza msomaji mwenzetu Jerome, changamoto zake ni mbili ya kwanza ni mbinu za kufanya biashara na kupata faida na ya pili ni jinsi ya kupata fursa kwenye eneo lolote la biashara. Tutaanza na changamoto ya jinsi ya kupata fursa za kibias